Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez pamoja na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), nchini Tanzania, Filiberto Ceriani Sebregondi (kulia) wakisaini hati ya mkataba wa kuyapatia Mashirika ya Umoja wa Mataifa Euro 200,000 kwa ajili ya Maendeleo Zitakazonufaisha wananchi wa Tanzania. (Picha Geofrey Adroph wa pamoja blog)
Balozi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), nchini Tanzania, Filiberto Ceriani Sebregondi (kulia) akibadilishana hati na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la Maendeleo (UNDP) nchini , Alvaro Rodriguez wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba wa kuyapatia Mashirika ya Umoja wa Mataifa Euro 200,000. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), nchini Tanzania, Filiberto Ceriani Sebregondi akifafanua jambo wakati wa hafla ya kutiliana saini mkataba wa kuyapatia Mashirika ya Umoja wa Mataifa ruzuku kwa ajili ya Shughuli za mendeleo hapa nchini.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akizungumza jambo mbele ya waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa (hawapo pichani) katika hafla ya kutiliana saini mkataba wa kuyapatia Mashirika ya Umoja wa Mataifa Euro 200,000.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali nchini wakirekodi tukio hilo.
Pichani
juu na chini baadhi ya wanahabari, wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa
Mataifa na wa Umoja wa Ulaya pamoja na wakuu wa Mashirika mbalimbali ya
Umoja wa Mataifa.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akibadilishana mawazo na Balozi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), nchini Tanzania, Filiberto Ceriani Sebregondi (katikati) baada ya kumalizika kwa hafla fupi ya kutiliana saini mkataba wa kuyapatia Mashirika ya Umoja wa Mataifa Euro 200,000.
Picha ya pamoja na mabango yenye malengo ya maendeleo endelevu SDGs.
Na Mwandishi wetu.
JUMUIYA
ya Ulaya (EU)imetiliana saini na Mashirika ya Umoja wa Mataifa yaliyopo
nchini Tanzania yanayofanya kazi kama shirika moja (One UN),ikiwa ni
ruzuku ya Euro 200,000 sawa na sh. Milioni 478,000,000 fedha taslimu za
kitanzania kwa ajili ya kushirikiana katika shughuli mbalimbali za
maendeleo zitakazonufaisha wananchi wa Tanzania.
Utilianaji
saini huo ulifanywa na Mratibu wa Mashirika ya UN nchini, Alvaro
Rodriguez na Balozi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), Filiberto Sebregondi.Aidha
utiaji wa saini hizo ulifanyika katika Ofisi za EU jijini Dar es salaam
na kushuhudiwa na wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya
Ulaya.
Akizungumza
wakati wa kutiliana saini Balozi wa Jumuiya ya Ulaya (EU), nchini
Tanzania, Filiberto Ceriani alisema Tanzania imefanikiwa kutengeneza
mfano wa namna bora Mashirika ya UN yanavyoweza kufanyakazi kama taasisi
moja katika kuboresha maisha ya watu.
Aidha
alisema ruzuku hii imetolewa kwa Mashirika ya Umoja wa Mataifa imelenga
kusaidia miradi ya pamoja kati ya Jumuiya ya Ulaya (EU) pamoja na
Umoja wa Mataifa hapa nchini.
Jumuiya
ya Ulaya (EU) nchini Tanzania imekuwa ikitoa ushirikiano katika program
kadhaa na mashirika ya Umoja wa Mataifa kama vile IOM, UNICEF, UNDP,
UNODC, UNHCR, FAO, UNESCO, IFAD, UN Women na WFP.
Naye
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Alvaro Rodriguez
akizungumza wakati wa kutiliana saini alisema fedha hizo zimelenga
kusaidia miradi ya pamoja ya EU na UN ya mawasiliano, uragibishi,
uimarishaji wa ufuatiliaji na uwazi.
Rodriguez,
alisema msaada huo ni muhimu katika ufanisi wa maendeleo kwa Tanzania
wakati nchi inajipanga kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu SDGs
ambapo amesema “Nchi ina Rais mpya na inahitaji kuwa ya kipato cha kati
sisi UN na washirika wetu ni vyema tukaunga jitihada hizi ili kusiwepo
na mtanzania atakayeachwa nyuma katika mchakato wa maendeleo,”
No comments:
Post a Comment