Wednesday, July 13, 2016

KUELEKA GULIO LA TANGAMANO TANGA

 Mwendesha mkokoteni mkazi wa Mabawa Tanga, akipita kwa tabu barabara ya 15 Ngamiani Tanga, kuelekea Gulio la Tangamano kupeleka Roba za Mitumba. Gulio la Tanga huwa kila siku ya Jumanne na Jumamozi na watu wengi hujinunulia bidhaa mbalimbali za majumbani na maofisini.
Gulio hilo ambalo awali ilisemekana kutaka kuhamishwa na kupelekwa Mwakidila ili kupisha ujenzi wa Gorofa la kisasa ambalo litakuwa na Ofisi mbalimbali hadi sasa hakuna taarifa yoyote.
Hata hivyo baada ya kutolewa kwa taarifa hiyo wafanyabiashara maarufu kama wamachinga walipinga kwa madai kuwa Mwakidila hakutakuwa na biashara kwa kile walichosema ni nje ya mji.
Uchunguzi wa ndani wa tangakumekuchablog imebaini kuwa dhamira ya ujenzi wa jengo la kisasa la kibishara bna maofisi upo pale pale ambapo pamoja na mambo mengine ni Sera ya jiji kupanua jiji ili kuepuka msongomano katikati ya jiji.



Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment