Ebola nchini Sierra leone
Ripoti moja imebaini kwamba karibia dola millioni 14 za kugharamia vita dhidi ya ebola nchini Sierra Leone hazijulikani zilipo.
Mkaguzi mkuu amesema kuwa wizara ya afya na kituo cha kitaifa cha kukabiliana na ugonjwa wa ebola zilienda kinyume na sheria.
Mkaguzi
huyo amesema kuwa taasisi hizo mbili zilishindwa kutoa stakabadhi za
karatasi zilizotolewa kununua ambulansi na kujenga kituo cha matibabu
ya ebola .
Ripoti
hiyo imesema kulikuwa na malipo ya dharura mara mbili kwa wabunge na
maafisa wa polisi na kwamba fedha zilipewa watu fulani badala ya
mashirika ambayo wangewakilisha.
Serikali haijatoa jibu lolote kuhusu ripoti hiyo.BBC
No comments:
Post a Comment