Tangakumekuchablog
Tanga, BIASHARA ya Utalii Mapango ya
Amboni Tanga imeathirika baada ya tukio la mapigano ya kurushiana risasi baina
ya majambazi na polisi lililotokea kijiji cha Mleni kilometa tano kutoka katika
vivutio hivyo.
Akizungumza
na Tangakumekuchablog leo, Mhifadhi Msaidizi Mapango ya Amboni,Tabu
Mtelekezo, alisema kwa sasa hakuna wageni wanaofika eneo hilo baada ya vyombo
vya habari kupotosha eneo halisi lilipotokea mapigano baina ya majambazi na
polisi.
Alisema
toka tukio hilo lilipotokea wamepata wageni 16 ambapo ni idadi ndogo sana
ikilinganishwa kabla ya tukio ambapo walikuwa wakipokea wageni 300 wa ndani na
nje ya nchi.
“Hivi
unavyoona hapa hakuna mgeni yoyote ambaye anakuja hapa na yumejikalia tu----hii
ni kutokana na baadhi ya vyombo vya habari kupotosha umma ya tukio lilipotokea
alisema Mtelekezo na kuongeza
“Tunaviomba
vyombo vya habari kuandika habari sahihi ya eneo la mapigano ya majambazi na
polisi kwani ni zaidi ya kilometa tano na sio hapa---kwa kweli limetuathiri
sana na hakuna mtu anaekuja hapa” alisema
Kwa upande
wa wafanyabiashara eneo la mapangoni na vijiji vya jirani na vivutio hivyo
wamelalamika kukosa wateja kutoka na biashara zao kutegemea wageni
wanaotembelea eneo la vivutio.
Mmoja wa
wafanyabiashara mwenye duka, Rojas Mkufya, alisema kabla ya vyombo vya habari
kupotosha umma wa tukio has lilipotokea walikuwa wakiuza zaidi ya shilingi
lakini mbili na kwa sasa wako wastani wa shilingi elfu hamsini.
Alisema
taarifa hizo zimewapotosha wageni ambao walikuwa wateja wakubwa na kuweza
kununua mahitaji mbalimbali yakiwemo vinywaji na vyakula na kwa sasa wamekuwa
wakiwategemea wateja wa mtaani peke yake.
“Maduka
yetu yamefifia kama unavyoona hapa hakuna hata mteja mmoja jambo ambalo sio
kawaida---tulikuwa tunauza hadi shilingi laki mbili kwa maduka haya rejareja ni
mauzo makubwa sana” alisema Roja na kuongeza
“Mapango
ya amboni yamekuwa yakitembelea na wageni wengi na hii ndio njia yao na
wamekuwa wakisimama wakinunua vinywaji na viburudisho vyengine kwa kweli
taarifa za upotoshaji wa vyombo vya habari vimetuathiri sana” alisema
Roja
Kwa upande
wake Chonge Maumba, amesema upotoshaji huo umewaathiri hadi wachimba kokoto na
mawe ambao pia walikuwa wateja wakubwa katika maduka yao.
Alisema
wachimbaji hao ambao idadi yao ni kubwa walikuwa wakiwaingizia mapato makubwa
kwa siku na hivyo kuvitaka vyombo vya
usalama kulimaliza suala hilo eneo la Mleni na wageni kuweza kufanya shughuli
zao za kitalii kama kawaida.
Kwa upande
wa mama lishe, Zahra Ali amesema hakuna mteja anaefika kunywa chai wala chakula
zaidi ya wenyeji na hivyo kupatwa na kigugumizi cha kufunga biashara au
kuendelea.
Alisema
awali walikuwa wakipika mchele kilo tano na chakula kumalika na kwa sasa
wamekuwa wakipika kilo mbili ambazo hakimaliziki kutoka na wateja kuwa
wachache.
“ Hapa
katika genge langu hakuna mteja zaidi ya wenyeji ambao wanakuja kunywa chai na
chakula kidogo jambo ambalo sio mazoea---hii ni kutokana na wageni kukacha kuja
Mapangoni baada ya taarifa kupotoshwa” alisema Zahra
Alisema
hali hiyo ambayo hawajui inaweza kuchukua muda gani huku familia zao
zikitegemea wageni na wafanyakazi wa kuchimba kokoto na mawe wanaotumilia njia
hiyo kukatisha.
Mwisho
No comments:
Post a Comment