Saturday, October 3, 2015

BARCELONA NAYO YADUNDWA

FC Barcelona hali mbaya, ninayo matokeo ya mechi yao dhidi ya Sevilla

Bado ni ngumu kutabiri matokeo ya mechi za Ligi Kuu mbalimbali duniani, kutokana na vilabu vingi kuwa vimejiandaa kiasi kwamba zile timu ambazo tunaziona kuwa bora kuliko nyingine huwa zinapoteza michezo katika timu ambazo huenda ukawa unaona ni kibonde kutokana na jina la timu hiyo kutokuwa maarufu masikioni mwa watu.
1704208-36082563-2560-1440
Klabu ya FC Barcelona ya Hispania imekutana na kipigo cha goli 2-1 dhidi ya klabu ya Sevilla, mechi ambayo ilichezwa katika uwanja wa Estadio R. Sanchez Pizjuan, FC Barcelona ambayo inaendelea na mechi za Ligi Kuu Hispania bila nyota wake Lionel Messi ambaye yupo nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki nane kutokana na kuwa majeruhi.
1703978-36077992-640-360
Dakika ya 52 ya mchezo Michael Krohn-Dehli alianza kwa kuiandikia goli la kwanza klabu yake ya Sevilla wakati ambao FC Barcelona wanajipanga namna ya kusawazisha goli hilo, Vicente Iborra dakika 6 baadae akafunga goli la pili kwa upande wa Sevilla na kuzidi kuidhoofisha FC Barcelona. Neymar pekee ndio alipata nafasi ya kuipatia FC Barcelona goli la kufutia machozi dakika ya 74 kwa mkwaju wa penati.
 Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment