Saturday, October 3, 2015

SELFIE KWANZA KISHA HUDUMA

Shabiki hakujali kuwa Ronaldinho kapata ajali wala nini alipofika ni mwendo wa Selfie

Wengi tunamfahamu Ronaldinho kwa uwezo wake mkubwa uwanjani hasa wakati alipokuwa anacheza bara la Ulaya katika vilabu vya FC Barcelona ya Hispania na AC Milan ya Italia. Ronaldinho kwa sasa yupo kwao Brazil alikuwa katika klabu ya Fluminense ya Brazil kabla ya kuachana nayo hivi karibuni na kubakia kuwa mchezaji huru.
Mshindi huyo wa Ballon d’or mara mbili ameingia kwenye headlines hivi karibuni baada ya kuachwa na timu ya Fluminense ikiwa ni miezi mitatu tu imepita toka asaini mkataba mpya na klabu yake. Stori inayoshangaza mtu wangu Ronaldinho aliliingiza gari lake katika shimo kwa bahati mbaya ni kama ajali nyingine za kawaida barabarani.
download (3)
Kama ambavyo tumezoea kuona sehemu nyingi duniani mahali ambapo inatokea ajali watu huwa wa kwanza kujitokeza kusaidia na kuangalia kama kuna uwezekano wa kutoa msaada, baada ya Ronaldinho kuingiza gari lake katika shimo, moja kati ya shabiki zake alitokea bila kuwaza kuwa ni ajali Ronaldinho amepata, jamaa cha kwanza ni alipiga selfie na Ronaldinho.
1
Kwa habari, matukio na mixchezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment