Ukali wa Jose Mourinho haukusaidia Chelsea kupata ushindi, haya ni matokeo ya mechi yao dhidi ya Southampton
Licha ya kusifika kuwa na uwezo wa kucheza na akili za wachezaji na makocha wa timu pinzani, kocha wa klabu ya Chelsea Jose Mourinho ameshindwa kuifanya klabu yake ibaki na point zote tatu katika uwanja wake wa nyumbani Stamford Bridge.
Klabu ya Chelsea ambayo ipo katika kipindi kigumu kwa mechi zake za Ligi Kuu msimu huu, imekubali kipigo cha goli 3-1 kutoka kwa Southampton. Mapema kabla ya kucheza mechi dhidi ya Southampton Mourinho aliripotiwa kuwafokea wachezaji wake kwa kutojituma, kitu ambacho bado hakijasaidia Chelsea kupata ushindi katika uwanja wake wa nyumbani.
Chelsea waliingia uwanjani wakiwa na hali ya kupata ushindi katika mechi hiyo, baada ya dakika 10 za mwanzo Willian kupachika goli la kwanza, dakika ya 44 Southampton walifanikiwa kupata goli la kwanza kupitia kwa Steven Davis, dakika ya 60 kipindi cha pili Sadio Mane akaongeza goli la pili kabla ya Graziano Pelle kuja kuhitimisha idadi ya goli 3-1 na kuifanya Southampton kuondoka na point tatu muhimu.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment