Monday, October 5, 2015

BRENDAN RODGERS ATIMKA BAADA YA KUFUNGISHIWA VIRAGO

Baada ya kufutwa kazi Brendan Rodgers aondoka Liverpool, huyu ndio anatajwa kuwa mrithi wake

Aliyekuwa kocha wa klabu ya Liverpool Brendan Rodgers kwa mara ya kwanza ameoneka hadharani na familia yake October 5, ikiwa ni siku moja imepita toka afukuzwe kazi katika klabu ya Liverpool kutokana na kutofanya vizuri kwa michezo kadhaa ya Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu.
2D1DEAFE00000578-3260454-image-a-18_1444056226671
Brendan Rodgers baada ya kufukuzwa kazi Jumapili ya October 4, ameamua kwenda Malaga kwa ndege binafsi ya kukodi akiwa na mpenzi wake Charlotte Hind wakiwa pamoja na binti yao. Uamuzi wa Rodgers kwenda Malaga Hispania haujajulikana kwa ajili ya mapumziko au tayari kapata kibarua sehemu nyingine.
2D1DEB0600000578-3260454-image-m-38_1444056852112
Brendan Rodgers alimaliza utawala wake wa miaka mitatu Anfield Jumapili ya October 4 baada ya kulazimishwa sare na wapinzani wao wa jadi Everton, katika mchezo ambao ulipigwa nyumbani wa Everton nakumalizika kwa sare ya goli 1-1.
2D1DEABE00000578-3260454-image-m-40_1444056921063
Majadiliano ya uamuzi wa kufutwa kazi kwa Brendan Rodgers yanatajwa kudumu kwa muda wa wiki moja na inatajwa kuwa alijulishwa kwa njia ya simu na Rais wa kampuni ya Fenway Sports Group  Mike Gordon ambaye pia ndio mmiliki wa Liverpool. Ikiwa ni siku moja imepita toka afutwe kazi kocha huyo, hawa ndio makocha saba wanaohusishwa kurithi nafasi yake Jurgen KloppCarlo Ancelotti, Frank de BoerWalter MazzarriJurgen KlinsmannRonald Koeman na Gary McAllister.
2D1DF7C900000578-3260454-image-a-33_1444056394085
Jurgen Klopp ndio kocha anayepewa nafasi kubwa ya kurithi nafasi ya Brendan Rodgers kati ya makocha saba waliyoorodheshwa
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment