Friday, October 2, 2015

TAARIFA YA WANAJESHI WAWILI WALIOANGUKA BAHARINI

TAARIFA KUHUSU NDEGE YA JESHI ILIYOPATA AJALI

NDEGE ya mafunzo ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), iliyopata ajali ikiwa na marubani wawili katika eneo la Silversands, Visiwa vya Bundya, katika Mwambao wa Bahari ya Hindi Kaskazini Mashariki mwa Jiji la Dar es Salaam.Taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano, Makao Makuu ya Jeshi, Upanga, ilisema marubani hao wanaendelea kutafutwa baada ya kuzama habarini.
Tukio hilo limetokea Oktoba mosi, mwaka huu, saa tatu 3:30 asubuhi ambapo marubani waliopotea ni Luteni Kanali Talkisiyo Ndongoro na Kapteni Gaudence Hamis.
Chanzo cha ajali hiyo ni hitilafu ya injini ambapo baada ya marubani kugundua hitilafu hiyo, walifanya juhudi za kujiokoa kwa kutoka katika ndege kwa Parachuti na kutua  baharini na kuzama. 
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment