Baada ya Liverpool kumtimua Brendan Rodgers huyu ndio kocha wao mpya
Ikiwa zimepita zaidi ya siku kadhaa toka klabu ya Liverpool ya Uingereza imfukuze kazi aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Brendan Rodgers,
kulikuwa na stori za makocha kadhaa kurithi nafasi hiyo kabla ya Al
Hamis ya October 8 uongozi wa klabu hiyo ulithibitisha kuwa kocha mpya
wa klabu hiyo ni Jurgen Klopp.
Jurgen Klopp amethibitishwa kujiunga na klabu ya Liverpool kama kocha mpya na kurithi mikoba ya Brendan Rodgers aliyetimuliwa kazi jumapili ya October 4 baada ya kutoka sare na wapinzani wao wa jadi Everton. Jurgen Klopp anajiunga na Liverpool kwa mkataba wa miaka mitatu, mkataba ambao una kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.
Kocha huyo anajiunga na Liverpool baada ya kuwa hana timu toka mwishoni mwa msimu uliomalizika aondoke katika klabu ya Borussia Dortmund na kukaa bila timu. Hata hivyo Jurgen Klopp ameweka rekodi ya kuwa kocha wa kwanza wa kijerumani kuifundisha Liverpool na kuwa kocha wa pili wa kijerumani katika Ligi Kuu Uingereza.
Klabu ya Liverpool toka imeanzishwa imewahi kufundishwa na makocha 19 na sasa Jurgen Klopp
ana ongezeka na kuwa wa 20. Kocha huyo wa kijerumani atatambulishwa
rasmi mbele ya waandishi wa habari Ijumaa ya October 9 katika mkutano na
waandishi wa habari.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment