Friday, October 9, 2015

MGOMBEA UBUNGE ARUSHA ACT WAZALENDO AFARIKI

Mgombea Ubunge Arusha amefariki, kingine ni hiki >> Ugonjwa? Kampeni kusimama?, Mazishi?

October 09 2015 Tanzania inaguswa na taarifa nyingine ya Majonzi kwenye Siasa, ambapo Mgombea mwingine wa Ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kwa Tiketi ya Chama cha ACT-Wazalendo, Estomih MALLAH amefariki Dunia baada ya kuugua na kukimbizwa Hospitali.
Taarifa ya kwanza ilisema kuwa Mgombea huyo amefariki katika Hospitali ya KCMC Moshi ambapo alikuwa akipatiwa matibabu…  Msemaji wa Chama cha ACT-Wazalendo, Khamis Abdallah amenifikishia taarifa nyingine kuhusu Kifo cha Mgombea huyo.
Tatizo lilianza October 06 2015 wakati anajiandaa kwenda kwenye Mkutano wa Mgombea Urais, alisema anajisikia vibaya kichwa kinamuuma… Hakuweza kupanda Jukwaani, akapelekwa Hospitali ya KCMC baada ya hali kuwa mbaya. Jana saa nane usiku tukatumiwa taarifa ya msiba.”
ACT Office
Kuhusu taratibu za Kampeni na Mazishi, haya ndio majibu ya Msemaji wa Chama- “Chama kimesimamisha Kampeni mpaka Jumapili, na tumeagiza Bendera za Chama zipepee nusu mlingoti kwenye Ofisi zote za Chama… Chama kitakaa na Familia kuangalia taratibu za msiba na Mazishi…“>>- Khamis Abdallah.
ACT Flag
Chama cha ACT-Wazalendo kimepata pengo kwenye nafasi ya Mgombea Ubunge Jimbo la Arusha Mjini, kingine kilichosemwa na Khamis Abdallah ni hiki hapa >>>Kampeni zimesimama, Tume ndio itakayotoa utaratibu wa kuendelea na Kampeni za Ubunge Jimbo la Arusha Mjini baadaye.”
RIP
 Estomih Jonas Mallah.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment