Monday, October 5, 2015

KAMANDA WA POLISI MKOA WA TANGA AWAPIGA MSASA VIONGOZI WA DINI NA WAANDISHI WA HABARI


Tangakumekuchablog

Tanga, KAMANDA wa polisi Mkoani Tanga, Zuberi Mombeji, amewataka viongozi wa dini na waandishi wa habari kuzitumia nafasi zao kuielimisha jamii katika suala zima la amani kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.

Akizungumza katika kongamano la miundombinu ya amani iliyoitishwa na ofisi yake  jana, kamanda Mombeji alisema viongozi wa dini na waandishi wa habari wako na nafasi kubwa kuhakikisha uchaguzi mkuu unafanyika kwa amani.

Aliwataka viongozi hao wa dini  kuwahubiria wafuasi wao suala zima la amani na kujitokeza kwa wingi kupiga kura na mara baada ya kumaliza kurejea katika shughuli zake za kujitafutia riziki.

“Tumekutana hapa kwa pamoja nyinyi waandishi wa habari na viongozi wa dini kwani muko na nafasi kubwa kwa jamii hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu “ alisema Mombeji na kuongeza

“Ndugu zangu waandishi wa habari ninyi ndio mmoja wa muhimili wa amani zitumieni kalamu zenu vizuri na kuacha ushabiki wa kisiasa na andikeni kile chenye faida kwa jamii” alisema

Kamanda aliwataka waandishi hao kuwa makini katika kuripoti habari zao kwani maadili yakikiukwa kunaweza kuleta athari na hivyo kuwa sababu ya amani kuvunjika.

Aliwataka kuandika habari nyingi za kuelimisha jamii  ikiwemo kuandika makala yakiwa na lengo zima la kuelekea uchaguzi mkuu na watu kujitokeza kwa wingi na kuitumia kila mtu haki yake ya kumchaguzi kiongozi anamfaa.

“Kuna baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikishabikia vyama na kusahau maadili ya habari----tutambue kuwa lolote linaloweza kijitokeza litamhusu kila mmoja” alisema Mombeji

Alivitaka vyombo hivyo vya habari kipindi cha kampeni kuelekea uchaguzi mkuu kuandika habari ambazo zitawaongoza wananchi na kujua wajibu wao siku ya kupiga kura na kusema kuwa wengi sheria ya uchaguzi hawazijui.

Alisema miongozi mwa sheria hizo ni pamoja na kutakiwa mpiga kura mara baada ya kuchagua mgombea anaemtaka ni kuondoka eneo la kupigia
                                             Mwisho


Viongozi wa dini Tanga wakiwa katika kongamano la miundombinu ya amani kuelekea uchaguzi mkuu October 25 ulioitishwa na ofisi ya kamanda wa polisi Mkoa leo.



 Sheikh wa Taasisi ya Bilal Muslim tawi la Tanga,  Mohammed Mbaraka akichangia wakati wa kongamano la wadau wa amani kuelekea uchaguzi mkuu October 25 liliandaliwa na ofisi ya kamanda wa poli Mkoa leo

1 comment:

  1. SHITTA-CHOMBO CHA WAISLAMU WOTE MKOA WA TANGA KINA TAKA AMANI NA SALAMA BA UTULIVYO MUDA WOTE WA MAISHA YA MTANZANIA NA MISIKITI HAITATUMIWA KAMA MAJUKWAA YA SIASA ZA MTU AU CHAMA-MKOA WA TANGA.

    ReplyDelete