Mipango mingine ya Bondia Manny Pacquiao ni yeye na Siasa, baada ya Ubunge anaingia na huku..
Jana jumatatu bondia maarufu duniani Manny Pacquiao
aliweka wazi mikakati yake ya kuingia kwenye siasa baada ya kutangaza
kuwania nafasi ya Useneta katika moja ya majimbo nchini kwake Ufilipino.
Staa huyo kwenye Mchezo wa Boxing
alitangaza kuwa atagombea nafasi hiyo katika uchaguzi mkuu utakaofanyika
mwaka 2016 ingawa bado hajaweka wazi atagombea kupitia chama gani.
Bondia huyo maarufu kama Pac Man alikuwa mmoja wa wawakilishi kwenye bunge la nchi hiyo baada ya kuchaguliwa na wananchi wa wilaya yake.
Pacquiao alifanikiwa kushinda mataji
nane ya dunia kupitia mchezo wa ngumi lakini alishindwa katika pambano
lake la mwisho dhidi ya mpinzani wake Floyd Mayweather, ikiwa ni moja ya mapambano ya kifahari kufanyika duniani katika jiji la Las Vegas, Marekani.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment