Tuesday, October 6, 2015

KOCHA NAE MAJERUHI LAKINI YUKO MZIGONI

Hata kama anaumwa mguu mechi dhidi ya Argentina imemlazimu kuingia na kibaiskeli ili afundishe kikosi chake

Da!!!! teknolojia inazidi kuturahisishia mambo mbalimbali kuwa rahisi kama utakuwa unakumbuka vizuri katika somo la sayansi shule ya msingi kuna kitu kilikuwa kinaitwa mashine tata yaani kwa maana yake kwa lugha rahisi ni kitu chochote chenye uwezo wa kurahisisha kazi. Basi stori ipo hivi kocha wa timu ya taifa ya Ecuador Gustavo Quinteros anauguza jeraha la mguu lakini aliendelea na kukinoa kikosi chake.
2D20514D00000578-0-image-a-3_1444126625211
Kocha huyo raia wa Argentina aliumia mguu wake September 16 wakati alipokuwa akicheza mpira na rafiki zake, Gustavo Quinteros ambaye anatarajia kupona baada ya mwezi, amelazimika kuingia uwanjani na kundelea kufundisha huku akiwa anatumia usafiri maalumu ni kama baiskeli au vipikipiki vidogo. Gustavo Quinteros alipewa ruhusu ya kuendelea kuifundisha timu yake inayojiandaa na michezo ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018.
2D205A5E00000578-0-image-a-2_1444126619682
Gustavo Quinteros ameingia na kifaa hicho ambacho kinakitenga kwa mbele na ametumia kitenga hicho kuweka clipboard yake ya kufundishia, Ecuador wanajiandaa na mchezo wake wa kwanza wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018 dhidi ya Argentina October 9 mchezo utakaopigwa mjini Buenos Aries Argentina, kabla ya siku nne baadae kucheza nyumbani dhidi ya Bolivia.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment