Huyu ndio mtoto aliyezaliwa na kuvunja rekodi ya kuwa na uzito mkubwa zaidi India..
Kwenye Kitabu cha Kumbukumbu kubwa za Dunia, Guinness World Records
kumbukumbu kubwa kuwekwa na mtoto aliyezaliwa na uzito mkubwa zaidi
iliwekwa mwaka 1955 na mtoto ambaye alizaliwa akiwa na uzito wa Kilo 10
Italy.
Rekodi nyingine kubwa kwenye Kumbukumbu
Marekani ni ya mtoto aliyezaliwa na uzito wa Kilo 6.8 mwaka 2014, lakini
India nao wana Rekodi kubwa iliyowekwa kwa watoto wachanga wanaozaliwa.
Mama Goga Bai amejifungua
mtoto wa kiume October 01 2015 na Rekodi ambayo mtoto wake ameiweka
India ni ya kuzaliwa na uzito mkubwa zaidi ambao ni Kilo 5.9.
Daktari mmoja amesema huyo mtoto amevuja
Rekodi ya kuzaliwa na uzito mkubwa zaidi kwa sababu wastani wa watoto
wanaozaliwa India ni kati ya Kilo 2.5 na kilo 3.5.
Mama huyo kajifungua salama kabisa na yeye pamoja na mtoto wake wako kwenye afya nzuri.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment