Tangakumekuchablog
Tanga, MGOMBEA,
Ubunge jimbo la Tanga mjini, Omari Nundu (CCM), amesema endapo atachaguliwa kwa
mara nyengine tena atairejesha mitaa ya namba kama zamani na kuwataka wananchi
kumchagua kwa kura nyingi.
Akizungumza katika mkutano wa
kampeni jana barabara ya 14 Ngamiani, Nundu alisema akichaguliwa atazirejesha
barabara za namba kwa kubandika namba kila barabara kama ilivyokuwa zamani ili
kuwarahisishia ufahamu wageni.
Alisema zamani mgeni akingia Tanga
hakuhitaji kuuliza kwani kila barabara na mtaa kuna vibati ambavyo
vinamuelekeza mtaa aliopo na kuwa rahisi kutambua aendako na kutokuwa na sababu
ya kuuliza.
Alisema kwa sasa barabara hizo
vibati vinavyoonyesha nambari za barabara zimeibiwa na kufanywa chuma chakavu
jambo ambalo wageni linawapa shida kujua barabara aliyo na kulazimika kuuliza
ambapo zamani zilikuwa zikiongoza.
“Nduguni nawaomba munichague tena
kwa kura za kimbunga ili nikamilishe adhma yangu ya kuwaletea maendeleo nikiwa
nanyi----miongoni mwa hayo ni kuzirejesha nambari za barabara kama ilivyokuwa
zamani” alisema Nundu na kuongeza
“Zamani mgeni hakuwa na shida ya
kukatisha mitaa kwani ilikuwa
inamuongoza kule aendako----- hivyo vimeibiwa na kufanywa chuma chakavu
na niwaahidi kuwa nitalirejesha jiji katika hadhi yake kama ilivyokuwa” alisema
Akizungumzia kuhusu huduma za
kijamii, Nundu alisema atahakikisha vijiji ambavyo havijafikiwa na huduma ya
maji safi na salama pamoja na umeme vinafikiwa ili kuleta maendeleo.
Alisema kwa kushirikia na Serikali
na wananchi ndani ya miaka mitano maji na umeme utakuwa umefika vijiji vyote na
hivyo kuwataka wananchi kumchagua kwa kura nyingi.
“Nichagueni mimi nimalize ahadi
zangu ambazo uchaguzi mkuu uliopita niliwaahidi na kuzitekeleza lakini badi
kiduchu-----hili linawezekana kama mutanichagua tena” alisema Nundu
Aliwataka wananchi kata ya Ngamiani
kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura na kurejea sehemu zao za kazi na
kusubiri matokeo na kuwaasa kuacha kudanganywa na kuacha kutopiga kura.
Mwisho
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment