Kingine kilichonifikia kuhusu hatma ya mwanariadha Oscar Pistorius…
Maisha ya mwanariadha maarufu Oscar Pistorius gerezani yameendelea kubaki njiapanda baada ya wasimamizi wa kesi hiyo kushindwa kufikia muafaka wa kumuondoa gerezani.
Jana bodi inayosimamia kesi yake ilikutana kwa lengo la kumtoa mwanariadha huyo lakini walishindwa kuafikiana.
Wakili wake Brian Webber ameiambia AFP kuwa rufaa yake ya kuachiwa imerudishwa tena kwa bodi ya usimamizi wa kesi hadi hapo itakaposomwa tena.
Mwanariadha huyo amefungwa kifungo cha miaka mitano jela baada ya kukutwa na hatia ya kumuua aliyekuwa mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Oscar pamoja na wakili wake na ndugu
zake wamekuwa wakijaribu kila liwezekanalo ili aweze kuwa huru lakini
mpaka sasa bado haijawezekana.
Mwezi August Oscar alikuwa aruhusiwe
kutoka jela lakini ikashindikana baada ya mwendesha mashtaka Michael
Masutha kukataa dakika za mwisho
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment