Sunday, October 4, 2015

MTIKILA AFARIKI KWA AJALI YA GARI CHALINZE

BREAKING: Mchungaji Christopher Mtikila wa DP amefariki.


Mwanasiasa mkongwe na Mwenyekiti wa chama cha kisiasa cha  DP Christopher Mtikila amefariki dunia alfajiri ya leo wakati akitokea Morogoro kuelekea Dar es salaam.
IMG-20151004-WA0009
Taarifa zilizotufikia kupitia kwa kamanda wa Polisi Pwani Jafari Mohamed amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na alifarika saa 12 kasorobo katika kijiji cha Msolwa, Chalinze akiwa kwenye gari ndogo huku wenzake watatu wakijeruhiwa vibaya.
IMG-20151004-WA0006
Gari aliyopata nayo ajali Mch.Christopher Mtikila
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment