Tuesday, October 6, 2015

MMEA UNAOKULA WADUDU WAHARIBIFU

Mmea unaokula wadudu

Mmea  unaokula wadudu unatumia nguvu za matone ya mvua ili kuwakamata wadudu hao,wanasayansi wamebaini.
Wanasayansi hao kutoka chuo kikuu cha Bristol wamebaini kwamba matone hayo ya mvua husababisha mtikisiko katika majani ya mti huo ambayo yana umbo la mtungi.
Hatua hiyo huwapeleka wadudu katika mfuniko wa mtungi huo wenye mtego, ambapo wadudu hao huzamishwa na kuliwa.
Matokeo ya utafiti huo yaliochapishwa katika jarida la PNAS yanatokana na kamera zenye kasi na zisizo na mtikisiko mkubwa.
Kwa matumizi ya vifaa hivyo ,daktari Ulrike Bauer pamoja na wenzake walirekodi kasi na mtikisiko unayoendelea katika majani ya mti huo baada ya kuangukiwa na matoni hayo ya maji.
Hatua hiyo ni ya kipekee miongoni mwa mimiea , Daktari Bauer anasema.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment