Tuesday, October 6, 2015

RUBANI AFARIKI WAKATI WA SAFARI ANGANI

Pale ambapo Rubani anafariki katikati ya Safari na ndege inalazimika kutua..


Dharura inaweza kutokea popote na wakati wowote, unaweza kupata picha hofu utakayokuwa nayo ikitokea mko katikati ya safari kwenye Ndege angani alafu Rubani anafariki !!
Ndege ya American Airlines iliyokuwa imetoka Phoenix kwenda Boston Marekani imelazimika kutua kwa dharura Uwanja wa Syracuse, New York baada ya Rubani wa Ndege hiyo, Michael Johnston kufariki… Kifo chake iilikuwa ghafla tu ambapo baada ya hali yake kuwa mbaya alianza kupata huduma ya msaada kutoka kwa mmoja ya wahudumu wa Ndege lakini muda mfupi baadae akafariki.
American Flight
Msemaji wa Shirika la Ndege la American Airlines amesema Ndege ilitua salama kwa sababu ndani alikuwemo pia Rubani msaidizi, na kilichosaidia pia ni Sheria inayolazimisha kila ndege kuwa na Marubani wawili ndani.
Ndege ilikuwa na jumla ya Abiria 147, mpaka sasa sababu ya kifo chake haijafahamika japo mkewe anasema huenda Michael Johnston alifariki kwa tatizo la pressure.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment