Mganga Mfawidhi wa hospital ya Mkoa wa Kigoma Dkt. Fadhil Kibaya amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Alisema hali za majeruhi mpaka sasa siyo nzuri sana kwani wengi wameumia sehemu za kichwa na mwilini.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Kigoma Ferdinand Mtui alisema chanzo cha ajali hiyo ni gari hilo la jeshi kushindwa kupanda mlima na kusababisha tairi mbili za nyuma kupasuka.
Alisema ajali hiyo imetokea katika eneo la Kasaka karibu na mizani ambapo lori hilo la jeshi lilikuwa likitoka mjini kwenda kambini likiwa limebeba makreti ya soda na unga.
Kwa habari, mayukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment