Thursday, November 5, 2015

MWANTUMU MAHIZA ATOA TAHADHARI YA KIPINDUPINDI, TANGA



Tangakumekuchablog
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahizza ametoa tahadhari kwa wananchi kutunza mazingira katika maeneo yao baada ya kitisho cha ugonjwa wa kipindupindu kuingia Mkoani humo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mwantumu amesema hadi sasa ugonjwa huo umepiga hadi jiji la Tanga hivyo kuziagiza taasisi za elimu na watu binafsi kutoa elimu kwa wananchi.
Amesema kufuatia kitisho hicho atafanya ukaguzi katika shule , vyuo na mikusanyiko ya watu wengi ikiwemo vituo vya mabasi na baraza za kahawa.
Amesema yoyote ambaye hatoweka mazingira ya usafi katika eneo lake atachukuliwa hatua za kisheria ikiwemo kutozwa faini ya papo kwa hapo au kupelekwa mahakamani.
Serikali Mkoani hapa imeweka makambi maalumu kwa wagonjwa wa Kipindupindu na kusema kuwa kuepuka ugonmjwa huo ni mtu mwenyewe kwa kuzingatia taratibu za usafi mtu eneo lake.
                                                    Mwisho
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment