Mfanyabiashara wa zao la embe,
Suleiman Said, soko la Mlango wa Chuma Masiwani Tanga, akitayarisha biashara
yake kusubiri wateja, kipindi hiki cha msimu wa maembe wakulima na
wafanyabiashara wamekuwa wakisaka masoko baada ya kutokuwa na soko la uhakika
hivyo kupatwa na kitisho cha kuwaozea mikononi.
Kwa muda mrefu wakulima wa matunda na mbogamboga wamekuwa wakiililia Serikali kuwajengea soko la uhakika la kuuzia mazao yao ili kuepuka kulanguliwa na watu wenye pesa kwa kuwauzia kwa bei ya kutupa.
Hata hivyo Serikali imekuwa ikifanya jitihada za kuhakikisha kilio hicho cha wakulima kinafikia kikomo na hivyo kuweza kuendeleza kilimo chao kutoka cha mazoea na kuwa cha kisasa.
No comments:
Post a Comment