Picha ya kwanza ya Jupiter yatolewa
Chombo cha anga za juu cha shirika la Marekani la NASA kilichopewa jina Juno kimetuma picha za kwanza za sayari ya Jupiter.
Moja
ya hizo, iliyotolewa na NASA Jumanne inaonesha sayari hiyo ikiwa
imezungukwa na miezi mitatu kati ya miezi yake minne mikubwa.Miezi inayoonekana ni Lo, Europa na Ganymede. Mwezi huo mwingine uitwao Callisto hauonekani.
Picha hiyo ilipigwa Jumamosi sayari Juno ilipokuwa inazunguka sayari hiyo ikiwa umbali wa maili milioni tatu.
Juno iliingia katika mzingo wa Jupiter wiki iliyopita na kuanza kuizunguka sayari hiyo ambalo pia hufahamika kama Zohali au Zozali.
Safari yake kutoka duniani hadi ilichukua miaka mitano.
Juno itachunguza na kupeleleza sayari hiyo kwa miezi 20, lengo kuu likiwa kusaidia wanasayansi kubaini asili ya sayari hiyo ambayo wanaamini inaweza kuwasaidia kuelewa zaidi asili ya mfumo wa jua.
Chombo hicho cha juu kilipokuwa kinaikaribia Jupiter, kamera zake na mitambo mingine muhimu vilizimwa kuzuia visiharibiwe na miali nururishi. Baadaye, vilifunguliwa.
Wanasayansi wanatarajia picha za karibu zaidi za Jupiter zitapokelewa mwezi ujao.
- Jupiter ina ukubwa mara 11 kuzidi Dunia na uzito wake ni mara 300 zaidi
- Sayari hiyo hutumia miaka 12 ya dunia kulizunguka jua; siku moja huko hudumu saa 10.
- Muundo wake ni kama wa nyota , sana haidrojeni na helium.
- Nasa inapanga kuitumia Juno hadi Februari 2018.
- Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment