Tangakumekuchablog
Tanga, WAZIRI
wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki, ameliagiza
Jeshi la Polisi na Vyombo vya Usalama kuwafichua watumishi hewa na wenye vyeti
feki.
Akizungumza na wakuu wa Idara na
watumishi mbalimbali wa Serikali na Taasisi za Umma jana, Kairuki alisema mbali
ya kupewa taarifa ya kuwepo kwa watumishi hewa Tanga 198 amedai anaamini wapo
wengi.
Alisema ili kuweza kuwafichua
ameliomba jeshi la polisi na vyombo vya usalama kusaidia ili kuwakamata na
kuwapeleka katika vyombo vya sheria kabla ya wao kujinasua.
“Naliomba jeshi la polisi na vyombo
vya usalama kusaidia kuwafichua watumishi hewa na wenye vyeti feki, tunaamini
tutawakamata na kuwapeleka mahakamani
kabla ya wao kujinasua” alisema Kairuki na kuongeza
“Tunatambua kuwa kuna watumishi
wenye dhamana ambao hawana sifa ila kwa kuwa na vyeti vyao feki wamejipatia
vyeo ambavyo wanashindwa kuongoza” alisema
Akizungumzia kuhusu maadili, Kairuki
aliwataka watumishi hao kuzingatia maadili ya kazi na kutunza siri za Serikali
na kusema kuwa yoyote ambaye atashindwa ni vyema kujiengua.
Alisema Wizara yake itahakikisha
kila mtumishi na mkuu wa Idara anaitumia vyema nafasi yake kwa kuwahudumia
wananchi kwa usawa bila ubaguzi ili kuondosha manung’uniko kutoka kwa wananchi.
Alisema kuna baadhi ya Idara
zimekuwa zikilalamikiwa kwa kushindwa kuleta uadilifu na usawa kwa utoaji wa
huduma hivyo kuagiza tabia hiyo kukomeshwa mara moja.
Alisema mkuu yoyote wa Idara ambaye atashindwa kuitumia nafasi
yake kwa uadilifu ajiengue mwenyewe
kabla ya fagio kumpitia kwa madai kuwa Serikali ya awamu ya tano haitakiwa
watumishi kufanya kazi kwa mazoea.
Aliwataka wananchi kutoa taarifa za
malalamiko katika Idara za Serikali na za Umma ili kukomesha ukiritimba na
manyanyaso na utoaji wa huduma kwa
upendeleo
Mwisho
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angela Kairuki, akizungumza na wakuu wa Idara
na watumishi wa mbalimbali wa Umma, ukumbi wa mikutano jengo la mkuu wa Mkoa wa
Tanga jana.
Wakuu wa Idara na Watumishi mbalimbali wa Umma,wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki, wakati wa kikao na wakuu wa Idara na watumishi mbalimbali wa Serikali na Umma wa Mkoa wa Tanga jana, kikao kilichofanyika jana ukumbi wa jengo la Mkuu wa Mkoa
No comments:
Post a Comment