Watu
kadha wanahofiwa kufariki baada ya ndege iliyotengenezewa Urusi kuanguka
muda mfupi baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Juba, Sudan Kusini.
Ripoti zinasema huenda watu 40 wamefariki, baadhi wakiwa watu
walioangukiwa na ndege hiyo ya kubeba mizigo ardhini.
Ndege
hiyo, iliyokuwa safarini kuelekea mji wa Paloch katika jimbo la Upper
Nile ilianguka kwenye ukingo wa mashariki wa Mto Nile. Maafisa bado
wanatafuta manusura. Msemaji wa rais wa Sudan Kusini Ateny Wek Ateny
ameambia shirika la habari la Reuters kwamba mhudumu mmoja wa ndege hiyo
pamoja na mtoto, ambao walikuwa kwenye ndege hiyo, wamenusurika.
Ubalozi
wa Urusi nchini Uganda, ambao pia husimamia Sudan Kusini, umesema
unawasiliana na maafisa wa serikali Juba kupata habari zaidi, kwa mujibu
wa msemaji wake Radmir Gainanov.
Ajali hiyo imetokea siku chache tu baada ya ndege nyingine ya Urusi kuanguka eneo la Sinai, Misri Jumamosi.
Chanzo:BBC
No comments:
Post a Comment