Alex Oxlade-Chamberlain awezesha Arsenal kulaza Reading
Reading karibu wasawazishe baada ya mpira wakupinduliwa, wake Callum Harriott kutua juu ya lango lililokuwa linalindwa na Emiliano Martinez.
Arsenal walitawala mechi kipindi cha pili na Oxlade-Chamberlain akaongeza bao la pili dakika ya 78 na kuwawezesha kumaliza mechi ya 14 bila kushindwa.
Oxlade-Chamberlain, 23, alikuwa amesumbuka kupata nafasi kikosi cha kwanza timu ya Arsene Wenger mapema msimu huu.
Amecheza dakika 90 mechi mbili pekee, lakini kutokana na uchezaji wake mzuri karibuni, amempatia Wenger kila sababu ya kumpa nafasi kikosini.
Matokeo ya mechi za EFL
- Arsenal 2-0 Reading
- Bristol City 1-2 Hull
- Leeds 2-2 Norwich
- (Leeds United wakashinda 3-2 kupitia penalti)
- Liverpool 2-1 Tottenham
- Newcastle 6-0 Preston
No comments:
Post a Comment