Bondia Mashali ameuawa siku chache baada ya kubadili dini, jina lake la kiislamu limetajwa
Wapenda ngumi nchini wako katika majonzi makubwa baada ya kifo cha bondia nyota, Thomas Mashali.
Mashali au Muhammad kama ambavyo anatajwa baada ya kusilimu bondia huyo inaelezwa kutoka vyanzo vya habari kuuwawa katika kifo cha kutatanisha.
Taarifa zimesema kuwa Mohammad alipigiwa kelele za mwizi na kuelezwa kuwa kupigwa hadi mauti kumfika.
Mashali ameuwawa katika moja ya viunga vya jiji la Dar es Salaam,
ikielezwa aliokotwa eneo la Kimara ingawa kuna wengine wanasema
ameokotwa eneo la Tabata.
Kitu ambacho Watanzania wengi hawakukijua ni kwamba, wakati mauti
yanamkuta, Mashali alikuwa amebadili dini siku chache, kutokuwa kuwa
Mkristo hadi Mwislamu, akaamua kuacha kutumia jina la Thomas na alikuwa
akitumia jina la Mohammed.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa (PST), Anthony Rutta amesema, Mashali kweli alibadili dini.
"Kweli alikuwa anaitwa Mohammed, hili alitueleza mwenyewe kwamba aliamua mwenye kwa hiari yake kuwa mwislamu," alisema Rutta.
No comments:
Post a Comment