Tangakumekuchablog
Tanga, KOCHA Mkuu wa Mgambo JKT, Athuman
Cairo , amewataka wachezaji wake kufanya mazoezi mfululizo asubuhi na jioni ili
kujiweka sawa kuweza kukabilia na mchezo wao na Mvuvuma FC ya Kigoma kesho uwanja wa Mkwakwani.
Akizungumza mara baada ya kumalizika mazoezi uwanja wa
Mkwakwani jana, Kaira alisema hataki kurejea makosa yaliyoilazimisha timu yake
kutoka kutoka suluhu ya kufungana bao moja moja.
Alisema yuko makini kuwaangalia wachezaji wake katika kila
aina ya mazoezi yakiwemo ya viungo na kasi ya uwanjani pamoja na kuwahi mazoezi
kwa wakati hivyo kuahidi kupata ushindi mnono.
“Kwa sasa nimefanya marekebisho kwa makosa yaliyojitokeza
wakati wa mechi yetu iliyopita na kulazimishwa kutoka sare, nimewaeleza kuwa
nitakuwa mkali kuona mchezaji hafuati maelekezo ninayotoa” alisema Caoro na
kuongeza
“Natambua ligi hii ni ngumu na kila timu imesajili wachezaji
wazuri na kujipanga, niko na imani na kikosi change lakini sitobweteka nataka
kila mmoja kujua wajibu wake uwanjani” alisema
Aliwataka washabiki wa mpira Tanga kuishangilia timu yake
uwanjani kwa wingi ili kuipa na kuzipa hamasa timu za Tanga ili kurejesha
makali yake kama ilivyokuwa msimu wa ligi uliopita.
Aliwataka kusahau machungu ya timu za Tanga kushuka daraja na
badala yake kuzipa moyo na hamasa kwa kujitokeza kw awingi uwanjani kwa
kuzishangiliwa kwa kutambua kuwa timu za Tanga ni za wana Tanga na zitaendelea
kuwa za wana Tanga.
Kwa upande wake, Kaptaini wa timu hiyo, Shai Mpala, alisema
wamejipanga vyema kuikabili Mvuvuma na kusema kuwa pointi tatu zitabaki
Mkwakwani ambapo hakuna majeruhi hadi muda huo.
Alisema mazoezi na maelekezo ambayo wamekuwa wakipatiwa na
makocha wao wamekuwa wakiyazingatia hivyo kuomba uzima hadi siku hiyo kwa madai
kuwa wako na hamasa.
“Tuko na hamasa na shauku ya mchezo ulioko mbele yetu na nina
imani kuwa kwa tulivyoiva ushindi utabaki hapahapa uwanjani, washabikiw awasiwe
na hofu ninachowataka wajitokeze kwa wingi.
Alisema ili kuweza kuibuka na ushindi amewataka washabiki
kujitokeza kwa wingi siku ya mechi ili kuwapa mori wachezaji uwanjani na
kuwashangilia kwa nguvu.
Mwisho
No comments:
Post a Comment