Tuesday, October 18, 2016

TATIZO LA KUOTA NYAMA PUANI

Tatizo la kuota nyama Puani

Nyama za puani ni nyama laini zilizoota na  kuning'inia  kwenye njia ya hewa na mianzi ya pua ambazo husababiswa na uvimbe wa muda mrefu kwenye mfumo wa upumuaji, pumu, maambukizi ya mara kwa mara, aleji na magonjwa mengine ya njia ya hewa.

Nyama zikiwa ndogo huwa hakuna dalili wala ishara zozote zinazoingilia mfumo wa upumuaji ila zinapokuwa kubwa uzuia hewa kuingia na kuharibu mfumo wa upumuaji sambamba na kushindwa kunusa, maumivu ya uso, maumivu ya meno ya juu, mafua, kukoroma, macho kuwasha na maambukizi ya mara kwa mara katika njia ya hewa.

MATIBABU YAKE
Matibabu ya tatizo ili huwa ni pamoja na dawa, kubadili mfumo wa maisha  na upasuaji kulingana na ukubwa au visababishi vya tatizo.

Dawa kama nasonex, cetirizine, antibiotiks huweza kutumika kwa nyia ya kunyunyuzia kwenye pua, vidonge au sindando ili kupuguza na kuzuia ukuaji wa nyama hizi huku zikisafisha mfumo wa upumuaji.

Upasuaji ufanyika endapo dawa zimeshindwa kuondoa tatizo ili na huwa ni upasuaji wa kutumia hadubini ya ndani kumuongoza daktari kuona kwenye njia ya hewa na miazi ya pua. Baada ya kufanya upasuaji utaweza kutumia dawa zilizotajwa juu hapo ili kuzuia kutokea tena kwa tatizo.
mgblog


No comments:

Post a Comment