Thursday, October 27, 2016

HADITHI, YAMENIKUTA SALMA MIE SEHEMU YA 24

HADITHI
 
YAMENIKUTA SALAMA MIE
 
ILIPOISHIA
 
“Ni uzee tu. Kila mahali panamuuma.Na presha yake pia iko juu” nikadanganya.Kwakuwa sikutaka tuendelee na mazungumzo yale nikamuuliza  “Kaka yako ameshalala?”
 
“Ameingia chumbani muda mrefu”
 
“Mmekula nini?”
 
“Tumekunywa chai.Nilikwenda kununua mkate”
Nikajidai kumuuliza  “Mmenibakishia na mimi?”
 
“Tumekuachia silesi zako”
 
“Mmefanya vizuri, njaa inaniuma”
 
Baada ya hapo tukabaki kinywa  tukiangalia ule mkanda.Kukaa kwangu pale na kuangalia huo mkanda ilikuwa ni kuvunga tu kwani nilijua nilikuwa nimechelewa kurudi na nilikuwa na ile hisi ya kutenda hatia.
 
Bila kupenda niliuangalia ule mkanda hadi ulipokuwa unakaribia kwisha Ibrahim akatoka na kumuuliza Abdul. “Shemeji yako hajarudi bado?”
 
SASA ENDELEA
 
“Kaka yako ameshalala?” nikamuuliza Zacharia.
 
“Ameingia chumbani muda mrefu”
 
“Mmekula nini?”
 
“Tumekunywa chai. Nilikwenda kununua mkate”
 
Nikajidai kumuuliza  “Mmenibakishia na mimi?”
 
“Tumekuachia silesi zako”
 
“Mmefanya vizuri, njaa inaniuma”
 
Baada ya hapo tukabaki kimywa tukiangalia ile kanda. Kukaa kwangu pale na kuangalia ile kanda ilikuwa ni kuvunga tu kwani nilijua nilikuwa nimechelewa kurudi na nilikuwa na ile hisi ya kutenda dhambi.
 
Ghafla Ibrahim akatoka mle chumbani na kumuuliza mdogo wake.
 
“Shemeji yako hajarudi hadi muda huu?”
 
Abdul akaniangalia kabla ya kumjibu.
 
“Amesharudi, tunaangalia kanda”
 
Ibrahim akaonekana kupata faraja kidogo. Akaniita
 
“Salma!”
 
 “Wasemaje?” nikamuuliza.
 
“Mbona umechelewa sana ?”
 
“Nimechelewa sana? Kwani nimerudi sasa hivi? Mdogo wako si amekuambia tunaangalia kanda!”
 
“Ulirudi mapema? Mimi sijui, sijakuona”
 
“Utaniona wapi wakati uko ndani?”
 
Nilitaka kumwaambia utaniona wapi wakati huoni lakini nikabadili maneno.
 
Akanyamaza kidogo kabla ya kuniuliza. 
 
“Unamuonaje mgonjwa?”
 
“Bado anaumwa” nikamdanganya
 
“Cha mno ni nini hasa” akaendelea kuniuliza
 
“Mwili wote unamuuma. Pia ana presha”
 
“Presha gani, ya kushuka au ya kupnada?”
 
“Presha ya kupanda”
 
“Sasa amepata tiba?”
 
“Alipelekwa hospitali, anatumia dawa”   
 
Nilipomjibu hivyo akanyamaza tena kidogo, kisha akaniambia.
 
“Mimi naenda kulala”
 
Sikumjibu kitu. Akageuka na kurudi chumbani. Kusema kweli nilikuwa nimemchukia. Nilikuwa nikimuona kama mtu anayenipotezea muda wangu bure.
 
Wakati alipotoka kule chumbani na kuja kuniuliza, nilidhani angegomba. Nilikuwa nikingoja aseme neno lolote la kunituhumu nimnyambue kisha ningetoka usiku ule ule na kurudi kwa Chinga.
 
Mkanda ulipokwisha nilikwenda mezani nikanywa chai na silesi walizoniachia kisha nikaingia chumbani.
 
Asubuhi kulipokucha wakati ninafanya usafi wa nyumba nilienda uani nikampigia simu Chinga kumsalimia.
 
Akafurahi nilivyompigia simu asubuhi ile.
 
“Umeshaamka au bado umelala?” nilimuuliza baada ya kukosa maneno ya kuzungumza.
 
“Bado niko kitandani”
“Kitandani hadi muda huu?”
 
“Ni harakishe nini, sina pa kwenda”
 
“Una raha mwenzetu. Natamani nije tulale sote”
 
“Sasa nani anakuzuia?”
 
“Si huyu ‘mnoko’ anayenipotezea muda wangu” nilimaanisha Ibrahim.
 
“Jana uliporudi alikuambia nini?”
 
“Hakuniambia kitu, si anajua nilikuwa kwa shangazi”
 
“Sasa mbona unasema anakuzuia usije huku?”
 
“Hanizuii lakini si ndiye kikwazo changu. Natamani niliue niondoke”
 
Chinga akacheka kwenye simu.
 
“Usimuue utapata hatia, tumia taratibu atakuacha tu. Hakuna ndoa ya lazima”
 
“Ataniacha lini wakati mimi nataka niondoke hata sasa hivi?”
 
“Usiwe na haraka hivyo. Mimi nitakusubiri tu”
 
“Si unataka kurudi Dar”
 
“Hata kama nitarudi Dar, sitakaa sana nitakuja tena kwa ajili yako”
 
“Nataka ukiondoka tuondoke sote. Hata kama sijapewa talaka, huyu mwanaume nitamuacha tu”
 
“Basi tutazungumza, si utakuja usiku?’
 
“Leo sitakuja,tufanye kesho ila nitakupigia simu usiku”
 
“Sawa”
 
Nilitegemea Chinga angekata simu lakini simu haikukatwa, nikamuuliza.
 
“Mbona hukati simu?”
 
“Kata wewe” akaniambia.
 
“Kata wewe bwana!” na mimi nikamwaambia.
 
Chinga akacheka kisha akakata simu.
 
Nilipokuwa narudi ndani nikamuona Ibrahim nyuma ya mlango akipapasa ukuta akielekea upande wa chumbani kwetu. Nikajiuliza ni kitu gani kilichomleta nyuma ya mlango?. Sikupata jibu. Lakini nilishuku kuwa pengine alikuwa akisikiliza nilivyokuwa ninaongea na Chinga.
 
Nikajiambia kama ametusikia atakuwa ameijua siri yangu wakati mimi sikutaka aujue uhusiano wangu na Chinga.
 
Ingawa sikuwa na uhakika kwamba alikuwa akitusikiliza au la lakini nilijiambia kama ametusikia nitajua kwani ni lazima ataniuliza.
 
Na nilingoja aniulize ndipo nimueleze wazi kuwa nilikuwa nimemchoka na nilihitaji kuondoka kwake, hivyo anipe talaka yangu.
 
Ibrahim akaingia chumbani na mimi nikaingia humo humo ili kama amesikia kitu aniulize. Lakini Ibrahim hakuniuliza chochote.
Ilipofika saa nne nilitoka bila kumuaga nikaenda sokoni.
Niliporudi niliingia jikoni. Nilikuwa nimenunua samaki,mchele na vitu vingine. Pesa ya Chinga ilikuwa inafanyakazi.
 
Nikaanza kupika. Hadi saa saba mchana wali ukawa tayari. Nikawatengea Ibrahim na mdogo wake kwenye meza na mimi kama kawaida yangu nilijipakulia kiasi changu nikaenda kukaa uani.
 
Wakati ninakula nilijiuliza, mbona Ibrahim hakuniuliza kitu wala hakuonesha kukasirika?.Huenda hakuyasikia mazungumzo yangu na Chinga. Moyo wangu ukapata faraja kidogo.
 
Ilipofika mida ya jioni nikamwaambia Ibrahim kuwa ninakwenda kwa Rita kuzungumza. Si kwamba nilikuwa nimebadilika na kuamua kumpa heshima yake ya kumuaga kila ninapotaka kutoka, lahasha. Kumuaga huko  kulikuwa ni kuzuga tu kama vile namfanya mjinga. Mbona nikiwa na safari zangu za maana nilikuwa simuagi!
 
Nilichukua muda mwingi nikiwa kwa jirani yangu Rita tukizungumza hili na lile lakini kubwa tuliloliongelea ni kuhusu uhusiano wangu na Chinga.
 
Kwa vile msimamo wa Rita ulikuwa nisiachane na Ibrahim kwa kuwa mimi ndiye niliyemsababishia matatizo ya macho, sikumueleza undani wangu kuwa nilitaka niolewe na Chinga kwa sababu angeupinga uamuzi wangu huo.
 
ITAENDELEA
 

No comments:

Post a Comment