Tuesday, October 25, 2016

MABALOZI NCHI 12 ZA ULAYA WAWASILI TANGA KUANGALIA FURSA ZA UWEKEZAJI

 Kaimu Meneja wa Bandari wa Bandari Tanga, Hendry Arika, (kushoto)  akimtambulisha kiongozi wa Mabalozi wa Jumuiya ya Ulaya wanaowakilisha nchi zao nchi, Roeland Vande Geer kwa Captain Bandari, Endrew Matiria wakati ulipofanya ziara yake Tanga kuangalia fursa za uwekezaji baada ya ujio wa mradi wa Bomba la Mafuta Tanga.
Mabalozi 12 kutoka nchi mbalimbali wamefika Tanga kuangalia furasa za uwekezaji kwa kutembelea Bandari ya Tanga, Bohari ya mafuta ya GBP  na eneo ambalo litajengwa bombala Mafuta kijiji cha Chongoleani.
Akizungumza katika mkutano na ujumbe huo, Meneja wa Bandari Tanga, Hendry Arika, alisema ujumbe huo umejionea kasi kuelekea ujenzi wa bomba la Mafuta na kuwataka wawekezaji wa ndani kuangalia namna ambavyo nao watawekeza.


 Kaimu Meneja Bandari Tanga, Hendry Arika, akiwafahamisha mabalozi wa nchi za Ulaya wanaowakilisha nchi zao nchini wakati walipotembelea Bandari ya Tanga kuangalia fursa za uwekezaji kufuatia ujio wa mradi wa bomba la mafuta Tanga.



 Mabalozi wakitembelea bohari ya mafuta bohari ya GBP.

  Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Tanga, Daudi Mayeji, akiwaonyesha mabalozi wa nchi  12 za Ulaya wanaoziwakilisha nchini zao nchini ramani ya eneo litakapojengwa bomba la mafuta kijiji cha Chongoleani Tanga ziara waliyoifanya leo.
 Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Hendry Arika akizungumza na waandishi wa habari leo eneo litakalojengwa bomba la mafuta kijiji cha Chongoleani Tanga wakati wa ziara ya mabalozi 12 kutoka Jumuiya ya Ulaya wanaowakilisha nchini zai nchini.
Kiongozi wa mabalozi wa nchi 12 Jumuiya ya Ulaya, Roeland Van Geer, akizunguza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya mabalozi hao Tanga kuangalia fursa za uwekezaji kufuatia ujio wa bomba la Mafuta

No comments:

Post a Comment