China yaongoza kwa uchangiaji wa viungo vya binadamu duniani..
October 18 2016, Mtu wako wa nguvu nimeipata ripoti hii kutoka
mkutano wa kimataifa wa uchangiaji viungo vya binadamu wa mwaka 2016
ambapo imeelezwa kuwa hadi kufikia tarehe 30 Septemba, 2016 watu 8,866
wa China walichangia viungo elfu 25 baada ya kufariki, na idadi ya
viungo vilivyochangiwa katika robo tatu ya mwanzo ya mwaka huu
imeongezeka kwa nusu kuliko mwaka jana kipindi kama hiki.
Ikiwa ni
mara ya kwanza kwa mkutano wa kimataifa wa uchangiaji na upandikizaji wa
viungo kufanyika nchini China, imeelezwa kuwa hali hiyo inatokana na
maendeleo ya kasi ya uchangiaji na upandikizaji wa viungo na kuendelea
kukamilika kwa mifumo husika katika miaka kadhaa iliyopita.
Taarifa ya
Mkurugenzi wa kamati ya afya na uzazi wa mpango ya China Li Bin
imesema, China imejenga kwa hatua ya mwanzo mfumo wa uchangiaji na
upandikizaji wa viungo vya binadamu ambao unafuata kanuni za kisayansi
na maadili ya kibinadamu, na pia unalingana na hali halisi na utamaduni
wa China.
>>>China
imekamilisha mfumo wa uchangiaji na ugavi wa viungo vya binadamu, sasa
imetimiza utaratibu wa kugawa viungo kulingana na mahitaji kwa njia ya
kompyuta, na vilevile China imeanzisha njia maalumu za kusafirishia
viungo ili kupunguza muda wa kuvifikisha kwa wenye mahitaji na kuokoa
maisha yao.
Aidha,
China pia imejenga mtandao wa usimamizi wa viungo, ili kuweza
kuvifuatilia na kuvisimamia wakati wote. Haswa katika mwaka 2015, China
imefanikiwa kuendeleza mageuzi kwa vyanzo vya viungo vya binadamu,
ambayo ni mafanikio ya kihistoria:- Li Bin
Ripoti
kutoka mkutano huo zinasema kuanzia Januari 1, 2016 China imeacha kabisa
kutumia viungo vya wafungwa waliohukumiwa adhabu ya kifo ili
kufanya upandikizaji na uchangiaji wa hiari wa viungo vya binadamu baada
ya kufariki.
Kwa mujibu
wa Katibu Mkuu wa Shirika la afya duniani WHO Bi. Margaret Chan
amepongeza mafanikio yaliyopatikana nchini China katika upandikizaji wa
viungo, Katibu huyo amesema China imetekeleza mageuzi kwa mwelekeo
sahihi na kwa ufanisi, na Shirika la afya duniani litaendelea kuunga
mkono kazi za uchangiaji na upandikizaji wa viungo nchini China.
millardayo
No comments:
Post a Comment