Tangakumekuchablog
Tanga, JESHI La Polisi Tanga limezuia
kufanyika mkutano mkuu maalumu wa Chama
Cha Wananchi (CUF) Leo ambao ungewajadili madiwani 12 ambao waliingia katika Baraza
la Madiwani na taarifa zilisema kuwa
Katibu Mkuu, Maalimu Seif Sharif Hamad angekuwepo.
Taarifa za jeshi la polisi kwa vyombo vya habari zimedai
kuwa kuzuiwa kwa mkutano huo ni kitisho
cha uvunjifu wa amani kutokana na kuwepo kwa makundi mawili yanayozozana.
Taarifa hiyo iliyotolewa na
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Tanga, Idd Abdalla, zimeongeza kuwa ukumbi
ambao mkutano huo ungelifanyika ni mdogo kutokana na wingi wa wanachama
ikikumbukwa kuwa juma lililopita mkutano wa chama hicho ngazi ya Wilaya
ulivunjika kwa vurugu.
Akizungujmza na waandishi wa habari,Mwenyekiti wa CUF Wilaya,
Rashd Jumbe, alisema kuzuiwa kwa mkutano huo kutofanyika lengo la chama la
kuwajadili madiwani hao upo pale pale.
Alisema kamati tendaji imependekeza madiwani 7 kati ya 12
kufukuzwa uanachama kutokana na kukiuka msimamo wa chama ambapo madiwani watano
wako katika uchunguzi.
“Mkutano wetu polisi wameuzuia lakini niseme kuwa msimamo wa
chama wa kuwafukuzwa wmadiwani waliokiuka msimamo watachukuliwa hatua na
kufukuzwa” alisema Jumbe na kuonmgeza
“Katika fagio hili mbunge pia yumo kwani nae alishiriki
kikamilifu pamoja na naibu meya, kwa sasa tunafanya utaratibu na jeshi la
polisi kufuata vigezo wanavyotaka ili kuufanya mkutano huo tena” alisema
Akizungumzia uimara na mshikamano ndani ya chama, Jumbe
alisema chama kiko imara na hakina mpasuko kama baadhi ya wapinzani wao
wanavyodai hivyo kuwataka wanachama kufanya subra kipindi hiki cha kuwajadili
madiwani waliokisaliti chama.
Mwisho
No comments:
Post a Comment