Hofu ya Coastal Union kucheza bila mashabiki au kuondolewa kabisa Mkwakwani yatawala
Hatma ya vurugu zilizotokea kwenye mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza kati
ya Coastal Union na KMC uliopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani, Tanga
itajulikana leo baada ya Kamati ya Saa 72 kuketi kujadili ripoti za
mchezo huo.
Hata hivyo kumekuwa na hofu kwamba, huenda Coastal Union inaweza
kuondolewa kwenye uwanja huo kutokana na tabia za mashabiki wake
kuwapiga waamuzi mara kwa mara.
Mchezo huo uliopigwa Jumapili iliyopita ulimalizika kwa vurugu kali kwa
mwamuzi wa kati, Thomas Mkombozi kushambuliwa kwa mawe na silaha
nyingine na mashabiki waliodhaniwa kuwa wa Coastal Union, waliomtuhumu
‘kuinyonga’ timu yao iliyochezea kichapo cha mabao 3-2.
Msemaji wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Alfred Lucas, amesema
pamoja na kusubiria maamuzi ya kamati hiyo, kanuni za wazi ni kwamba
iwapo ripoti zitabainisha mashabiki ndio wenye makosa, basi Coastal kuna
hatari ya kucheza mechi zilizobaki bila mashabiki ama kuhamishwa kutoka
uwanjani hapo.
Mashabiki wa Coastal Union wamekuwa wakikumbana na shutuma ya kuwapiga
waamuzi wa soka kwa madai ya kuwa wanaibana timu yao kwa makusudi.
mgblog
No comments:
Post a Comment