HADITHI
YAMENIKUTA SALMA MIE
ILIPOISHIA
Nikashuka kutoka kwenye gari na kutembea kuelekea nyumbani.
Nilikuta mlango wa mbele ukiwa umefungwa. Nikabisha. Zacharia
akaja kunifungulia, nikaingia.
“Habari ya saa hizi?” akanisalimia.
“Nzuri” nikamjibu huku nikizuga kwa kuangalia kwenye runinga.
“Unatazama kanda?” nikamuuliza.
Niliona deki imewashwa na kuonesha filamu za kina Kanumba.
“Ndiyo shemeji” Zacharia akanijibu huku akifunga mlango kisha
akaniuliza.
“Vipi hali ya shangazi?”
“Bado anaumwa” nikamjibu huku nikiketi kwenye sofa.
Nikajifanya nataka kuangalia ile kanda. Zacharia aliondoka kwenye
mlango naye akaja kuketi.
“Kwani ana tatizo gani?” akaniuliza.
“Ni uzee tu. Kila mahali panamuuma. Na presha yake pia iko juu”
nikadanganya. Kwa kuwa sikutaka tuendelee na mazungumzo yale nikamuuliza.
“Kaka yako ameshalala?” nikamuuliza Zacharia.
“Ameingia chumbani muda mrefu”
“Mmekula nini?”
“Tumekunywa chai. Nilikwenda kununua mkate”
Nikajidai kumuuliza “Mmenibakishia na mimi?”
“Tumekuachia silesi zako”
“Mmefanya vizuri, njaa inaniuma”
Baada ya hapo tukabaki kimywa tukiangalia ile kanda. Kukaa kwangu
pale na kuangalia ile kanda ilikuwa ni kuvunga tu kwani nilijua nilikuwa
nimechelewa kurudi na nilikuwa na ile hisi ya kutenda dhambi.
Ghafla Ibrahim akatoka mle chumbani na kumuuliza mdogo wake.
“Shemeji yako hajarudi hadi muda huu?”
SASA ENDELEA
Bila kupenda niliangalia ile kanda, hadi ilipokuwa inakaribia
kwisha Ibrahim akatoka na kumuuliza zacharia..
“Shemeji yako hajarudi bado?”
Chinga akapiga funda jingine la bia. Alipoirudisha birauli
aliniambia. “Hatutakosa njia nyingine. Nakupa muda uendelee kufikiri
lakini jaribu kumshinikiza akupe taraka”
“Wewe utakuwa hapa Tanga mpaka lini?”
“Sina muda mrefu. Naweza kuondoka siku yoyote nitakayoamua”
“Basi tuendelee kufikilia njia nyingine. Kwa vile sina nia ya
kuendelea kuishi naye kama hata niacha yeye
nitamuacha mimi!”
“Lakini umenipenda?” Chinga akaniuliza ghafra. Macho yake
yalionesha kuwa ulevi ulikuwa umeanza kumchukua.Iliwezekana alianza kunywa muda
mrefu.
“ Kama nisingekupenda nisingekuja huku” nikamjibu
“ Kama ni kweli kunywa bia kidogo”
“Nimekuambia situmii”
“Onja kidogo”
“Nitaonya siku nyingine”
“Basi njoo uketi hapa”
Alimaanisha nikaketi naye kitandani.
“Hapa nilipokaa panatosha”
Chinga akainuka na kunifuata akanishika mkono na kuniinua.
‘Mbona uko hivyo Salma? Hebu twende tukakae pale”
“Chinga utasababisha nichelewe nyumbani” nikajidai kulalamika huku
nikimfuata kwenye kitanda. Nikaketi na yeye akaketi”
“Wewe umeshaamua kuwa na mimi unajali nini kuchelewa. Wewe ni
wangu tu au si kweli?”
Nikanyamaza kimya na kubaki kumtazama machoni.
Akatabasamu na kunipitishia mkono kiunoni “Unamacho ya
kimahaba kweli!” akaniambia kasha akanibusu midomoni.
Kilichofuatia baada ya hapo sitakisema. Niaibu
Ilikuwa saa nne ikikaribia kuwa na nusu Chinga aliponirudisha
nyumbani. Nilimwaambia asimamishe gari nyumbni kwa Mwanaisha ili Ibrahim na
mdogo wake wasijue kuwa nimeletwa na gari
Chinga akanipa shilingi laki moja kabla sijashuka kwenye gari
“Ahsante” nikamwaambia kabla ya kuagana naye. Nikashuka na
kutembea kuelekea nyumbani. Niliposhuka tu Chinga akaondoka na gari
Nilipofika nyumbani mlango wa mbele ulikuwa
umefungwa.Nikabisha.Abdul akaja kunifungulia, nikaingia
“Habari ya saa hizi?” akanisalimia
“Nzuri” nikamjibu huku nikizuga kwa kuangalia kwenye luninga
“Unatazama kanda?” nikamuuliza
Niliona deki imewashwa na kuonyesha filamu za akina Kanumba
“Ndiyo shemeji” Abdul akanijibu huku akifunga mlango.
“Unamuonaje shangazi?’
“Bado anaumwa” nilimjibu huku nikiketi kwenye sofa.
Nikajifanya nataka kuangalia ule mkanda
Abdul aliondoka kwenye mlango naye akaja kuketi
“Tatizo la shangazi ni nini?” akaniuliza
“Ni uzee tu. Kila mahali panamuuma.Na presha yake pia iko juu”
nikadanganya.Kwakuwa sikutaka tuendelee na mazungumzo yale nikamuuliza
“Kaka yako ameshalala?”
“Ameingia chumbani muda mrefu”
“Mmekula nini?”
“Tumekunywa chai.Nilikwenda kununua mkate”
Nikajidai kumuuliza “Mmenibakishia na mimi?”
“Tumekuachia silesi zako”
“Mmefanya vizuri, njaa inaniuma”
Baada ya hapo tukabaki kinywa tukiangalia ule mkanda.Kukaa
kwangu pale na kuangalia huo mkanda ilikuwa ni kuvunga tu kwani nilijua
nilikuwa nimechelewa kurudi na nilikuwa na ile hisi ya kutenda hatia.
Bila kupenda niliuangalia ule mkanda hadi ulipokuwa unakaribia
kwisha Ibrahim akatoka na kumuuliza Abdul. “Shemeji yako hajarudi bado?”
Itaendelea
No comments:
Post a Comment