Hii ndio idadi ya Watanzania wanaoishi na VVU
Serikali
imesema kuwa licha ya Mipango mikakati na mbinu madhubuti ambazo
zimetekelezwa bado takwimu zinaonesha kuwa kiwango cha maambukizi
miongoni mwa makundi maalum na yale yaliyo katika hatari zaidi ya
kuambukizwa VVU yapo juu.
Hayo yameelezwa katika taarifa iliyotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo
ya Jamii,Jinsia, Wazee na Watoto ambapo imesema ilianza kutoa huduma za
VVU na UKIMWI kwa makundi hayo maalum tangu mwaka 2010 baada ya kufanya
tafiti na kugundua kuwa kiwango cha maambukizi ya VVU kiko juu kwenye
makundi hayo.
Serikali imeyataja makundi yaliyopo hatarini zaidi kwa maambuki hayo ni
pamoja na wasichana na wavulana, walio katika umri wa balehe, watoto
yatima na watoto walio katika mazingira hatarishi, wanaume wanaofanya
ngono na wanaume wenzao, wanawake wanaofanya ngono kinyume na maumbile,
watu wanaotumia dawa za kulevya kwa njia ya kujidunga sindano.
Takwimu zinaonyesha kuwa takribani watu MILIONI MOJA NA LAKI NNE
(1,400,000) wanaishi na VVU nchini Tanzania ambapo, watu 839,574
wanapatiwa tiba ya dawa za kupunguza makali ya VVU zinazotolewa katika
vituo ambapo takriban vituo 4,000 vilikuwa vinatoa huduma hiyo nchi
nzima hadi kufikia mwezi Juni mwaka huu (2016)
source mgblog
No comments:
Post a Comment