Utafiti umeonesha upigaji mpira kwa kichwa una madhara
Watafiti kutoka
chuo kikuu cha Stirling huko Scotland wamegundua kuwa kumbukumbu ya
mchezaji wa mpira wa miguu inaweza kuathirika kwa upigaji wa mpira kwa
kutumia kichwa kwa muda mfupi.
Wanasema kuwa ufanyaji kazi wa
kumbukumbu hupungua kwa kati ya asilimia 41 na 67 kulingana na idadi ya
upigaji wa mpira kwa kutumia kichwa na hurudi katika hali ya kawaida baada ya
masaa 24.Mmoja wa watafiti hao Dr Magdalena Letswaart amesema ingawa mabadiliko sio ya kudumu lakini kuna umuhimu katika Afya ya Ubongo, hivyo wachezaji wanatakiwa kuwa makini kwa upigaji huo na kinatokea ndani ya ubongo.
Chuo hicho kimesema kuwa watafanya uchunguzi ili kujua kama madhara yatakua ya kudumu baada ya kucheza mara kwa mara mpira wa miguu na kutumia kichwa.
BBC
No comments:
Post a Comment