Tangakumekuchablog
Tanga,WAFANYABIASHARA wa pikipiki maarufu
kama (Bodaboda) Tanga, wameitaka Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania
(TRA) na halmashauri ya jiji la Tanga kuwapunguzia wingi wa kodi vyenginevyo biashara
hiyo inaweza kuwa ngumu kwao.
Wakizungumza katika kikao
kilichowakutanisha, jeshi la polisi, mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na
halmashauri ya jiji la Tanga leo, wafanyabiashara hao wamesema kukuwa kwa
sekta hiyo isiwe kafara kwa kuongezewa kodi.
Wamezitaja kodi hizo zikiwa ni
shilingi 25,000 wanazotakiwa kulipa Mamlaka ya Mapato, kodi ya
Insuarence, kodi ya pikipiki (motavehecle), na kodi ya fere
instungsher pamoja na kodi ya maegesho ya pikipiki zao ambazo zote hizo ni
vigumu kulipika kulingana na kipato chao.
“Waheshiwa meza kuu hamuoni kodi hizi
kama munatubebesha wakati hatustahili kulipishwa wakati sisi ni wavuja
jasho----kuna watu wako na miradi mingi na mikubwa lakini hawana utitiri wa
kodi kama za kwetu” alisema Fadhili Mfaume
“Jambo ambalo kama Serikali haitoweza
kulivalia njuga ni kuruhusu kodi za kuzuka kama hii ya maegesho----vijana wengi
wametokana na matukio mabaya ya uvutaji bangi na uporaji na leo unamfukuza
aende wapi” alisema
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa
bodaboda na bajaj
Wilaya ya Tanga, Daudy Bilaly,
amewataka madereva wa pikipiki na bajaj kuwa na umoja na mshikamano miongoni
mwao ili kuweza kuiendeleza sekta hiyo na kuwa ya mfano.
Alisema kuna baadhi ya maeneo
madereva wa bajaj na pikipiki wamekuwa hawana uelewano jambo ambalo ni baya
katika sekta hiyo na hivyo kuwataka kuwa kitu kimoja.
“Jamani sekta yetu kila siku inakuwa
kwa kasi na imekuwa mkombozi kwa watu ambao hawana kazi----hii imewavuta pia
watu ambao walikuwa waporaji na wavuta bangi na kuona huku ndiko kuliko na
riziki ya halali” alisema Daudy
Aliwataka madereva hao kila mmoja
kuwa mlinzi wa mwenzake na yoyote ambaye ataonekana kutumiliwa na watu
waovu na kutoa siri za umoja wao katika kukabiliana na matukio ya kihalifu
aripiotiwe katika vyombo husika na kuchukuliwa hatua za kisheria.
Akizungumza katika kikao hicho,
kamanda wa usalama barabarani Mkoa wa Tanga, Abdi Issango, aliwataka madereva
wa pikipiki kuacha mtindo ulioibuka wa kupakiza abiria zaidi ya mmoja na kusema
kuwa msako wa kukomesha tabia hiyo utaanza mara moja.
Alisema ndani ya msako huo atakamatwa
abiria ambaye amepakizwa mshikaki na ambaye hakuvaa kofia ngumu (helment) na
kumtoza faini ya papo kwa papo au mahakamani.
“Kila siku tumekuwa tukipiga kelele
kukemea uvunjifu wa sheria za usalama barabarani lakini elimu hiyo huingia
sikioni na kutokea sikio la pili----sasa dawa imeiva na tunaingia barabarani”
alisema Issango
Aliwataka abiria kugoma kupakizwa
mishakaki na kuhakikisha dereva anakuwa na kofia mbili na endapo amembaini kuwa
amelewa kugoma kwani lolote laweza kujitokeza mbele ya safari ikiwemo
kuibiwa au kumsababishia ajali.
No comments:
Post a Comment