Monday, January 26, 2015

SOMA HABARI KUU ZILIZOPEWA UZITO MAGAZETI YA LEO, TZ

Mkusanyiko wa Stori zilizopewa Headlines kwenye Magazeti ya leo January 26, 2015 nimekuwekea hapa

tisa
MTANZANIA
Mmiliki wa Continental Night Club na Hunters club Omprakash Singh, ametiwa hatiani na Serikali  kutaifis baada ya kupatikana na hatia ya kuwaingiza nchini wasichana 22 kutoka India na Nepal kwa ajili ya kuwafanyisha kazi ngumu na biashara ya ngono.
Singh alitiwa mbaroni na mahakama ya Kisutu mwishoni mwa wiki mbele ya hakimu mkazi, Devotha Kisoka.
Hakimu Kisoka alimtia hatiani mshtakiwa baada ya kukiri kosa linalomkabili la kuwaingiza nchini wasichana hao, aliowatumikisha kazi ngumu na alikua akiwauza kwa ngono na kujipatia fedha.
“Unatakiwa kuwalipa wasichana wote 22 mishahara yao yote na utawalipia usafiri wa kuwarudisha kwao:- Kisoka.
Magari yaliyotaifishwa na Serikali  yanadaiwa kutumiwa na mtuhumiwa kuhamisha wasichana hao kutoka sehemu moja na kwenda kuwauza sehemu nyingine.
Hakimu alisema endapo Mshtakiwa atashindwa kulipa faini atakwenda jela miaka 10.
MTANZANIA
SIKU moja baada ya aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, kutangaza kujiuzulu kutokana na kashfa ya uchotwaji wa zaidi ya Sh bilioni 300 katika Akaunti ya Tegeta Escrow, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imesema suala hilo bado ni bichi.
Pamoja na hali hiyo, PAC imesema hadi sasa Serikali imetekeleza maazimio manane ya Bunge kwa asilimia 35.
Akizungumza jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), Zitto Kabwe, alisema kati ya maazimio manane yaliyopitishwa na Bunge hadi sasa ni matatu pekee yaliyotekelezwa.
Alisema suala la Akaunti ya Tegeta Escrow ni kubwa kuliko Profesa Muhongo, hivyo watu waliodhani kuondoka kwake litakuwa mwisho wanajidanganya.
PAC itaendelea kupaza sauti ili maazimio yatekelezwe. Watu waliodhani kuwa akitoka (Profesa) Muhongo basi suala hili limekwisha wanajidanganya. Suala hili ni kubwa zaidi ya Muhongo:-Zitto.
vya kijinai kuhusiana na Miamala ya Akaunti ya Escrow na watu wengine watakaogundulika kufuatia uchunguzi unaoendelea kuhusika katika vitendo vya jinai.
Zitto alisema mpaka sasa ni vidagaa tu wamefikishwa mahakamani kuhusiana na suala hilo.
MTANZANIA
WAJUMBE wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, wamewataka Watanzania kuikataa Katiba inayopendekezwa kwa kuwa haikuzingatia masilahi ya Watanzania.
Waliyasema hayo juzi katika ukumbi wa MCC, mjini Musoma kwenye mdahalo wa kujadili na kuelimisha wananchi kuhusiana na mchakato wa kupata Katiba Mpya na kuwataka kupiga kura ya hapana.
Akizungumza katika mdahalo huo, aliyekuwa Mjumbe wa Tume hiyo, Joseph Butiku, alisema mchakato wa kukusanya maoni ya Katiba, haukuandaliwa kienyeji bali ulipitishwa kisheria ambapo kazi hiyo ilifanyika kwa kujali masilahi na haki za Watanzania kwa vizazi vijavyo.
Kuipigia kura ya Ndiyo Katiba inayopendekezwa ni kuuza utu wako, Katiba hiyo haikidhi hata kidogo masilahi ya wananchi ni Katiba inayoandaliwa kwa ajili ya masilahi ya watu fulani fulani:-Butiku.
Alisema Tume yao haikupindisha maoni ya wananchi ila baada ya kuikabidhi tu, wapo wajanja kwa sababu zao waliweka mambo yao kwa kupindisha baadhi ya vipengele wanavyotaka wao huku wakitupilia mbali maoni halisi ya wananchi.
MWANANCHI
Panga pangua ya saba ya Baraza la Mawaziri iliyofanyika juzi imefikisha Mawaziri 61 waliotemwa, kujiuzulu au kufariki dunia tangu Rais Jakaya Kikwete aingie madarakani mwaka 2005, huku mawaziri 16 wakihimili mawimbi hayo hadi sasa.
Katika mabadiliko hayo saba yaliyofanywa katika kipindi cha miaka tisa, wako waliobadilishwa wizara, kupandishwa kutoka naibu waziri kuwa waziri kamili, huku sura mpya zikiingizwa.
Mabadiliko hayo yalitokana na mawaziri kutakiwa kuwajibika kutokana na kashfa mbalimbali, huku mengine yakitokana mawaziri kufariki na moja likitokana na Waziri Asha-Rose Migiro kuteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Katika panga pangua hiyo, mawaziri 16 wamefanikiwa kudumu katika baraza hilo tangu Rais Kikwete aingie madarakani ambao ni Sofia Simba, Profesa Mark Mwandosya, Stephen Wasira, Dk Hussein Mwinyi na Dk John Magufuli.
Wengine ni Profesa Jumanne Maghembe, Dk Shukuru Kawambwa, Hawa Ghasia, Dk Mary Nagu na Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye kabla ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo, alikuwa naibu waziri na baadaye waziri wa Tamisemi.
Mawaziri wengine waliopo sasa ambao mwaka 2005 walikuwa manaibu mawaziri ni Gaudencia Kabaka, Bernard Membe, Celina Kombani, Christopher Chiza na Mathias Chikawe.
Naibu waziri pekee ambaye alikuwamo katika baraza la mawaziri la kwanza la Rais Kikwete akiwa na wadhifa huohuo ni Dk Makongoro Mahanga ambaye sasa ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira.
MWANANCHI
Mwenyekiti wa CCM wa tawi la Texas, Houston nchini Marekani, Simon Makangula amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja na nusu jela na kulipa faini ya zaidi ya Sh92.4 milioni kwa kosa la kughushi nyaraka za ulipaji wa kodi.
Makangula ambaye ni mmiliki wa kampuni ya kutoa huduma za malipo ya kodi iitwayo Mshale Investment & Tax Service, alihukumiwa Ijumaa katika Mahakama ya Wilaya na Jaji Gray Miller kwa udanganyifu huo wa kuwasaidia wateja wake kughushi nyaraka za kodi ya mapato, kwa mujibu wa tovuti ya click2houston.com.
Wakili wa serikali nchini humo, Kenneth Magidson pamoja na Lucy Cruz, wakala maalumu wa kitengo cha uchunguzi wa makosa ya kihalifu katika masuala ya mapato ya Marekani, kwa nyakati tofauti waliiambia mahakama kuwa Makangula alimsaidia mmoja wa wateja wake ambaye ni raia wa Marekani kutayarisha malipo ya kodi yasiyo halali.
Sambamba na kifungo cha mwaka mmoja na nusu, pia Makangula anatakiwa kulipa faini ya Dola 51,645 sawa na Sh92.4 milioni.
Oktoba 15, mwaka jana, Makangula alikiri kosa hilo mbele ya hakimu Miller na kuwa malipo ya kodi hiyo yalikuwa na udanganyifu katika vipengele kadhaa, yakiwamo katika makadirio na idadi ya wategemezi wa mlipakodi, mambo yaliyosababisha hasara ya Dola 9,731 za Marekani (Sh17.3 milioni).
MWANANCHI
Mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngasa amelizua jipya baada ya kubainika kuikimbia timu hiyo na kwenda Afrika Kusini kufanya majaribio katika klabu moja ya huko.
Awali, Ngasa alikosekana katika timu hiyo kwa wiki moja na uongozi wa timu hiyo ukieleza kwamba anamuuguza ndugu yake ambaye ni mgonjwa.
Katibu wa Yanga, Dk Jonas Tibohora alisema Ngasa aliondoka katika timu hiyo akiomba ruhusa maalumu ya kumuuguza ndugu yake, lakini uongozi wao umepata taarifa kwamba yuko Afrika Kusini akisaka timu ya kumsajili bila ya ruhusa ya klabu yao.
Tibohora ambaye kitaaluma ni daktari wa Sayansi ya Michezo alisema taarifa hizo walizipata kutoka kwa baadhi ya wadau wa klabu yao ambao wamemwona mshambuliaji huyo nchini humo huku klabu inayotajwa kwamba ndiyo inataka kumsajili ni Free State Stars, ambayo iliwahi kumfanyia majaribio mwaka jana.
Alisema kwa sasa wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na endapo watabaini ukweli katika utovu huo wa nidhamu wa mshambuliaji huyo, mara baada ya kurudi watakutana naye huku pia kuna uwezekano wa kuishtaki klabu ambayo ibainika amekimbilia.
NIPASHE
Wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuanzia mwaka 2000 hadi 2014,  wanatarajia kuandamana tena keshokutwa kwenda Ikulu jijini Dar es Salaam kuwasilisha kilio chao cha kukosa ajira kwa muda mrefu.
Vijana hao wameamua kuandamana kwenda kuwasilisha kilio chao hicho kwa Rais Jakaya Kikwete baada ya  kuandika barua tatu kwenda Ikulu  bila  kujibiwa.
Akizungumza kwenye mkutano wa vijana hao Mwenyekiti wa Umoja huo,  George Mgoba,  alisema vijana wengi wamekuwa wakipelekwa kwenye mafunzo ya JKT  na kuahidiwa kupatiwa ajira na serikali huku wakiishia mitaani.
Jumatano  tutaandamana kwenda Ikulu kumuona Rais na kumfikishia kilio chetu cha kukosa ajira kwa miaka yote hiyo kwani tunaamini wanaomwakilisha wanamdanganya kwa kudai kuwa vijana wote waliomaliza JKT wameajiliwa sehemu mbalimbali kitendo ambacho siyo:-Mgoba
NIPASHE
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimewaomba wanafunzi wa elimu ya juu nchini kujitokeza kugombea nafasi za uongozi kupitia chama hicho.
Rai hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Stephen Wasira, mjini hapa katika hafla ya kuwapokea wanachama wapya 300 wa tawi la Chuo Kikuu cha Biashara na Ushirika Moshi (MUCO).
Wasira aliwaomba wanafunzi wa  MUCO, Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Stephano Moshi (SMUCCo), Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya na Tiba (KCMC), Chuo Kikuu cha Kikatoliki -Mwenge), Chuo Kikuu Kishiriki cha Theolojia (Mwika) na Chuo cha Kimataifa cha Usimamizi na Utunzaji wa Wanyamapori (Mweka), kukibeba chama hicho kwa kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi za ubunge kwenye maeneo ambayo yanaongozwa na vyama vya upinzani.
Hata hivyo, Wasira ambaye pia ni mlezi wa CCM Mkoa wa Arusha hakuwapo katika hafla hiyo, lakini aliwakilishwa na Katibu wa Chama hicho mkoa wa Arusha, Kinam’hala Alphonce.
HABARILEO
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amewataka Watanzania kutoa taarifa kuhusu makusudio ya kuuza nyumba za Serikali na mashirika ya umma, kutokana na madeni mbalimbali ili ziweze kukombolewa kabla ya kuuzwa.
Akizungumza Ikulu Dar es Salaam juzi, Balozi Sefue alisema kumejitokeza mtindo wa kukamata nyumba za Serikali na mashirika ya umma na kuzipiga mnada, kutokana na madeni yanayodaiwa kwa Serikali au mashirika hayo.
Sisi tumeona hii si sawa, unakuta nyumba ya Serikali inaweza kuwa na thamani labda ya Sh bilioni moja inauzwa kwa Sh milioni 100…mkiona nyumba ya Serikali inauzwa, toeni taarifa tuikomboe:-Sefue.
Alisema baada ya kuikomboa, watendaji husika walioachia nyumba ya Serikali ikataka kupigwa mnada, watashughulikiwa kwa uzembe baada ya kukomboa nyumba husika.
Balozi Sefue pia aliwataka Watanzania kuepuka kununua nyumba za umma, kwa kuwa hata baada ya ununuzi, Serikali haitakubali, bali itatafuta namna ya kukomboa nyumba yake.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,tangakumekuchablog

No comments:

Post a Comment