
Ulishawahi
kujiuliza jina lako lina maana gani au limetokana na nini? wengi
tumekuwa na majina ambayo hatujui maana yake na mengi yakiwa ni common,
lakini kuna mengine ambayo ni ya kipekee kwa mfano majina ya watoto wa
mastaa wa Marekani
Kim Kardashian anayeitwa ‘
North West’na mtoto wa
Beyonce ‘Blue Ivy’, ni majina ambayo inasemekana hayajawahi kusikika sehemu nyingine.

Kampuni moja huko
Sweeden ya
Erfolgswelle, ina
uwezo wa kubuni jina la mtoto wako ambalo linakuwa la kipekee na huwezi
kulikuta sehemu nyingine duniani, ambapo team ya watu 31 hukutana na
ndani ya masaa 100 jina hilo linapatikana, awali yanaletwa majina 15
yenye hati miliki na kukaguliwa na wataalam wanne ili kuthibitisha jina
hilo halifanani na jina lingine wala kutumiwa na mtu mwingine.
Kabla ya kusajiliwa jina hilo linaangaliwa katika tafsiri kumi
kuhakikisha kuwa halitafsiriki kwenye lugha yoyote ile wala halina maana
ya kitu chochote, baadae unafanyika utafiti wa kuangalia soko la jina
hilo ambapo hujaribishwa kwa kundi la watu 780, ili kuangalia kama
watalipenda kabla ya kulipitisha na kulisajili kisha kulipa kiasi cha
dola £21,000 ambazo ni zaidi milioni 33 za Kitanzania.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment