TANGAKUMEKUCHABLOG
Tanga, MEYA wa jiji la Tanga, Omar Guledi,
ametoa agizo kwa mabalozi wa nyumba kumi
na wenyeviti wa Serikali za mitaa kuwahamasisha wananchi kuweka mazingira ya
usafi maeneo yao na atakaekaidi achukuliwe hatua za kisheria.
Akizindua
mradi wa utunzaji na uhifadhi wa mazingira kwa kata ya Nguvumali na kushirikisha
viongozi wa kata, Serikali za mitaa na viongozi wa dini leo, Gulledi alisema
magonjwa ya miripuko na homa za mara kwa mara hazitoisha hadi jamii yenyewe
itakapobadilika juu ya usafi wa
mazingira.
Alisema kufuatia
kukaribia kwa msimu wa mvua ni wajibu wa kila kaya kuweka mazingira ya usafi
katika maeneo yao ikiwa na pamoja na kuifanyia usafi mifereji iliyoziba ili
kuwa rahisi mvua inaponyesha maji kutembea.
“Kwanza
niipongeze Asasi ya Nguvumali commity development of invironment kwa kubuni
jambo hili ambalo liko na faida ya kila mtu----mazingira yetu bado hayaridhishi
na kuna kitisho cha mvua kubwa mbele yetu” alisema na kuongeza
‘Tumesikia
kutoka kwa wataalamu wetu kuwa kuna mvua kubwa zinatarajia kunyesha na kama
hatutaweka maeneo yetu katika usafi tutajazana mahospitalini kwa kuugua
magonjwa ya miripuko” alisema Gulledi
Alisema ili
kuweza kulifanikisha zoezi hilo ni wajibu wa viongozi wa dini na Serikali
kuielimisha jamii kuweka mazingira ya usafi na yoyote ambaye atakuwa kikwazo
awajibishwe kwa mujibu wa taratibu na sheria.
Kwa upande
wake, Katibu wa Asasi ya Nguvumali Commity Development of Enviromment (NCDE),
Frank Mgunda, alisema kuongezeka vitendo
vya uharibifu wa mazingira katika vyanzo vya maji na uchimbaji wa madini katika
misitu.
Alisema Asasi
hiyo itafanya kampeni ya nyumba kwa nyumba kutoa elimu ya mazingira kwa kuanzia
mjini hadi vijijini kabla ya msimu wa mvua kuanza kunyesha ikiwa na pamoja na
vijiji vinavyoishi kandokando ya vyanzo vya maji na misitu.
“Sisi
tumedhamiria hasa kutoa elimu ya mazingira kwani kama yanavyonekana bado
hayaridhishi na tuko katika hatari ya kukumbwa ukame miaka ya mbele na maeneo
yetu kuwa jangwa baada ya kukithiri ukataji wa miti na uchimbaji wa madini
holela .
Alisema
elimu hiyo itakuwa ya kila kaya pamoja na kupita katika shule za msingi na
sekondari lengo likiwa ni kuhakikisha mazingira yetu yanakuwa katika hali ya kuridhisha.
Mwisho
No comments:
Post a Comment