Real Madrid ‘yauza’ uwanja wake .
Mabingwa wa ulaya Real Madrid wamekubali kuuza haki za kuupa jina uwanja wao wa nyumbani kwa familia ya falme za kiarabu ya Emirates ambapo sasa uwanja huo utabadilishwa jina na kuitwa Abu Dhabi Bernabeu .
Emirates imekubali kulipa kiasi cha paundi milioni 15 kwa mwaka ili kubadilisha jina uwanja huo katika mchakato ambao ulihusisha kampuni za Microsoft na Coca-Cola .
Uwanja huo ulizinduliwa rasmi mwaka 1947 huku ukipewa jina la mwenyekiti wa zamani wa klabu hiyo Santiago Bernabeu Yeste na kwa sasa unatarajiwa kupewa jina la Abu Dhabi ambalo litadumu kwa muda unaotajwa kuwa miaka 20 .
Uwanja huo una uwezo wa kuchukua watu wapatao 81,044 na umekuwa moja kati ya viwanja vya kihistoria ulimwenguni kote tangu kuanzishwa kwake .
Real Madrid wamekuwa na uhusiano na kampuni ambalimbali za falme za kiarabu ambapo mwaka jana walitia saini mkataba wa udhamini wa jezi na kampuni ya usafiri wa anga ya Fly Emirates na pia inaendesha mradi wa ujenzi wa kisiwa cha kifahari huko Dubai .
Yote haya mtu wangu unayapata kupitia www.tangakumekuchablog.spot.com
No comments:
Post a Comment