Unajua kuna nchi zinapiga marufuku watoto kupewa baadhi ya majina? Yako hapa…
Huku kwetu tuna utaratibu wa kuwapa
watoto wetu majina tunayopenda, yapo majina ya watu maarufu kama
viongozi, wanasoka, waigizaji na wengineo.
Kuna hizi nchi ambacho wao wamepiga marufuku baadhi ya majina kupewa watoto, list ni hii hapa.
New Zealand: Msajili wa Vizazi, Vifo na Ndoa nchi hii ameagiza baadhi ya majina kupigwa marufuku ikiwemo majina haya; Majesty, Queen Victoria, Lucifer na jina la Mafia No Fear.
Venezuela: Wao wamezuia matumizi ya jina la Superman kwa kuwa ni gumu kulitamka.
Denmark: Wametoa list
ya majina rasmi ambayo yako zaidi ya 7,000 mtoto akizaliwa anachaguliwa
jina kati ya majina hayo, moja ya majina yaliyozuiwa huku ni jina la
Monkey.
Brazil: Jina lililozuiwa huku ni jina la Saddam Hussein.
Mexico: Wamepiga marufuku mtoto kupewa majina ya Scrotum, Terminator, Burger King, Hitler na Virgin.
Uturuki: Mahakama imezuia mtoto kupewa jina la Osama Bin Laden
Portugal: Wao wamezuia jina la Tom.
Mfano hii ingekuja Bongo, majina gani ungependa yazuiwe wasipewe watoto wetu?
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia, www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment