Taarifa iliyotolewa na Serikali kuhusu ishu ya kukamatwa kwa Prof. Lipumba na wafuasi wake
Katika kikao cha Bunge siku ya jana January 28 Mbunge James Mbatia aliomba mwongozo ndani ya kikao cha Bunge kuhusu ishu iliyojitokeza juzi Dar ambapo Prof. Lipumba na baadhi ya wafuasi walikamatwa na Jeshi la Polisi.
Waziri wa Mambo ya Ndani alitoa majibu ya Serikali kuhusu ishu hiyo; “Mheshimiwa
Mbatia jana ametoa malalamiko kuwa katika kadhia hii Polisi wametumia
nguvu nyingi kuliko ilivyotakiwa, malalamiko haya ni mazito na Serikali
haiwezi kuyafumbia macho, kwa hiyo pamoja na uchunguzi unaofanya na Tume
ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, ninaagiza idara ya malalamiko
ndani ya Wizara kufanya uchunguzi kuhusu matumizi ya nguvu na ziada na
ikithibitika kuwa kuna Polisi walitumia nguvu nyingi zaidi dhidi ya raia
basi tutachukua hatua… Jeshi la Polisi halipaswi kutumia nguvu kuliko
zinazohitajika katika kuwakamata watuhumiwa wa makosa ya jinai, halipo
kwenye sheria, halipo kwenye Police General Orders“– Waziri Mathias Chikawe.
“Serikali
inawaomba radhi wananchi wote waliokumbana na kadhia hii bila wao
kujihusisha na kuwasihi wananchi kujiweka mbali na matukio yote ya
uvunjifu wa sheria, Jeshi la Polisi halitamuogopa wala kumuonea haya mtu
yoyote yule litatimiza wajibu wake kwa mujibu wa sheria.
“Polisi
watumie nguvu stahiki kwa tukio stahiki.. Polisi wetu wanawajibu wa
kuwalinda Watanzania wote na mali zao zote, kwa nguvu zao zote“– Mathias Chikawe.
No comments:
Post a Comment