Kumekuchablog
Tanga,POLISI Wilayani Korogwe Mkoani
Tanga, wamemkamata kondakta wa basi, Abdalla Kayomba (37) ambaye anasadikiwa
kuwa ndie msafirishaji mzoefu wa mihadharati aina ya mirungii kati ya
Kilimanjaro na Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake jana, Kaimu kamanda wa polisi Mkoani Tanga, Juma Ndaki, alisema
tukio hilo lilitokea usiku wa leo saa 6 kwenye kizuizi cha polisi kijiji cha
Chekelei Tarafa ya Mombo Wilayani Korogwe.
Alisema wakati wa kukamatwa
kwake kijana huyo alikutwa na kilo 35 za mirungi ambayo alikuwa ameificha
chini ya uvungu wa lori na kuweka katika magunia mawili ya mkaa .
“Kwanza baada ya polisi kumuona tu
walimuweka chini ya ulinzi kwani alikuwa akisakwa kwa udi na uvumba----wakati
wa mahojiano alifichua siri na kueleza bayana kusafirisha kilo 35 za mirungi”
alisema Ndaki na kuongeza
“Polisi walipoiona tu sura yake
walimkwida na kumuweka chini ya ulinzi----nae hakufanya shida kwani alikuwa
akijua kuwa anawindwa na sasa anahojiwa kutoa taarifa ili kuuzima mtandao wa
usafirishaji mihadharati” alisema
Alisema wakati polisi wakifichua
mirungi hiyo ambayo ilikuwa imefichwa katika magunia ya mkaa ilikuwa vigumu
kuigundua lakini walipatwa na hofu baada ya kusikia harufu kali iliyoasghiria
mirungi.
Katika hali nyengine, kaimu kamanda
wa polisi aliwataka wananchi wanaoishi kandokando ya milima ya Usambara
Wilayani Korogwe na Lushoto kutoa taarifa za watu wanaojishughulisha na kilimo
cha bangi.
Alisema kilimo hicho kimekuwa
kikishamiri katika Wilaya hizo na hivyo kutoa wito kwa wakulima waliobadilisha
aina ya kilimo na badala yake kulima bangi kuwa msako wa kuwasaka uko karibu.
“Natoa wito kwa wakazi wanaoishi
karibu na milima ambayo yunadhani kuna watu wamebadilisha aina ya kilimo na
kulima bangi kuwafichua na kutupa taarifa----polisi imejipanga kufanya msako
usiku na mchana” alisema Ndaki
Alisema tabia ya watu kulima bangi
badala kilimo cha chakula kunaifadhaisha jamii kwani eneo hilo kila mwaka
hukumbwa na njaa huku chanzo kikiwa ni wakulima kubadilisha kilimo.
No comments:
Post a Comment