
Jumanne
ya January 27 kwenye 255 ya leo inahusu swala la wasanii kutoko
Morogoro kupenda kukaa mkoani humo tofauti na wasanii wengine, ambapo
msanii
Stamina amezungumzia sababu
ya yeye kupenda kukaa Moro ni kutokana na maisha kuwa rahisi ingawa
mzunguko wa hela ni mdogo lakini maisha ni rahisi nani na ni mji
uliotulia tofauti na Dar ambapo mzunguko wa hela ni mkubwa na maisha
yako juu.

Baada ya Msanii
Jux
kwenda China kusoma inasemekana kuwa star huyo anafanya mambo mengine
na sio shule peke yake, kwa kuwa hajawahi kuonyesha picha yoyote akiwa
darasani au mazingira ya shule, msanii huyo amesema kuwa ni kweli
anasoma na hawezi kupiga picha ili kuonyesha watu kwa kuwa mazingira ya
shule hayaruhusu.

Story ya mwisho kusikika inamhusu muigizaji
Wema Sepetu baada ya gazeti moja kuandika kuwa anamdai shilingi milioni 10 aliyekuwa mpenzi wake
Diamond Platnumz, Meneja wake
Martin Kadinda
amesema kuwa swala hilo limemchafua Wema kwa hiyo analitaka Gazeti hilo
limuombe radhi na watoe tamko kuwa habari hiyo haikuwa ya kweli,
akizungumzia swala la kuachana kwao amesema
Wema hajampa taarifa zozote juu ya kuachana kwao ila hakuna hasara yoyote kwa kuwa kila mtu anaendelea na shughuli zake.
Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment