Leo January 31, STORY kubwa kutoka zilizopewa uziti magazetiya leo,TZ
MWANANCHI
Wabunge wameendelea kuwalipua mawaziri, huku wakimtaka Waziri wa Fedha, Saada Mkuya kufukuzwa kutokana na kukiuka Katiba, huku Mbunge Andrew Chenge akikumbana na kadhia ya kudaiwa kuwa anahusika kwenye kila mikataba mibovu, jambo lililosababisha Chenge kusimama na kutoa kauli ya kutaka ‘kuheshimiana’.
Hayo yalitokea Bungeni Dodoma wakati
Wabunge wakichangia taarifa za Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali
(PAC) na ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) ya mwaka ulioishia Juni
30 mwaka 2014.
Mkuya alitajwa
kubadili matumizi ya fedha zilizotengwa na Serikali kwa ajili ya
matumizi mengine, kitendo kinachomaanisha kuwa alivunja Katiba.
“Fedha
ambazo ziko kwenye ring fence (mfuko maalumu), hazitakiwi kutumika kwa
matumizi mengine kwa mujibu wa sheria. Kwa mujibu wa Katiba, Waziri
umevunja Katiba kwa mujibu wa ibara ya 135 na ibara ya 136 ni Tanzania
peke yake (Waziri Mkuya) unabaki salama. Hupaswi hata kupewa heshima ya
kujiuzulu, unafukuzwa kazi,” – Esther Bulaya.
Bulaya,
ambaye amekuwa mmoja wa wabunge wachache kutoka chama tawala wanaoihoji
Serikali, alisema wizara hiyo imeshindwa kukata fedha kwa ajili ya
chai, suti na sambusa na badala yake inakata fedha zilizokuwa ziende
kupeleka umeme vijijini.
Bulaya alikuwa akizungumzia Sh180.7
bilioni zilizokusanywa kulipia gharama za mradi kutokana na mauzo ya
mafuta ili ziweze kupeleka umeme vijijini.
Wakati wa kuhitimisha mjadala wa ripoti
hizo, Naibu Waziri wa Fedha (Sera), Mwigulu Nchemba alikiri kuwa wizara
iliyumba katika eneo hilo kutokana na hali ya kifedha ya Serikali.
“Mwaka huu ni hapa tu ambako tuliyumba,
(katika) eneo hili la matumizi ya fedha za miradi,” alisema Mwigulu na
kuongeza kuwa wizara yake inaandaa utaratibu utakaowezesha makosa hayo
kutojirudia.
MWANANCHI
Hofu imetanda kwa wazazi wa watoto ambao
wanasoma shule za msingi za Kabasa A na B Wilaya ya Bunda, Mara baada
ya kubuka kwa ugonjwa wenye dalili za kupanda ‘mapepo’ ambao unawaathiri
wanafunzi wa kike pekee.
Kutokana na ugonjwa huo kuhusishwa na
Imani za kishirikina uongozi wa Wilaya uliwataka viongozi wa kijiji
kukaa na wazee wa kimila ili kumaliza tatizo hilo.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya hiyo,
Boniface Maiga alisema Serikali haiamini ushirikina, kwa kuwa tatizo
limeanzia kwenye jamii basi jamii hiyo hiyo inapaswa kumaliza tatizo
hilo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kabasa B
alisema ugonjwa huo ulianza kati ya January 21 na 28 huku wakidhani kuwa
ugonjwa huo ni Malaria.
NIPASHE
Sakata la uchotwaji wa zaidi ya Shilingi
bilioni 300 kwenye akaunti ya Tegeta Escrow limeibuka tena bungeni na
kuzua malumbano makali baina ya Mwanasheria Mkuu mpya wa Serikali,
George Masaju na Mbunge Tundu Lissu ambaye alimwambia Masaju kuwa ni
mshauri wa serikali na si mshauri wa Bunge kuhusu masuala ya kisheria.
Wakati huohuo Lissu alisema licha ya
Bunge kumwondoa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kuwafukuza mawaziri,
waliochukuliwa hatua ya kufikishwa mahakamani ni watu wadogo waliopewa
milioni 80, huku wale waliogawana mabilioni ya fedha wakidunda mitaani.
“Watu wanafanya makosa makubwa dhidi ya
umma hakuna hatua inayochukuliwa, waheshimiwa wabunge mnaweza mkauliza,
lini mtu amewahi kuwajibika, nani kachukuliwa hatua, yupi amefungwa,
tunajua wanajiuzulu ili wakafaidi matunda ya wizi wao, sheria zetu
zinasema wajiuzulu, wafilisiwe, washitakiwe na wakipatikana na hatia
wafungwe, nani ameshitakiwa, kufilisiwa au kufungwa?”—Tundu Lissu.
Mbunge huyo alisema kuwa Bunge
liliazimia majaji waliohusika na sakata hilo Bunge wawajibishwe, lakini
Rais Kikwete hajawachukulia hatua kwa madai kuwa majaji hao wanatakiwa
kuchukuliwa hatua na mahakama, huku akishangaa nani anayemshauri Rais
masuala ya kikatiba na sheria.
“Maazimio ya Bunge lako ni kwamba
serikali ilete taarifa ya utekelezaji maazimio kabla ya kumalizika kwa
Bunge la Bajeti lakini hata kabla halijaanza… kanuni zinakataza
kumhusisha mheshimiwa Rais kujenga hoja kwa namna ya kejeli, kwa hiyo
mimi naomba kushauri kuwa tunapopata fursa ya kuchangia tujikite kwenye
hoja yetu na tutumie lugha ya staha kwa sababu ndivyo kanuni
zinavyoelekeza,” Mwanasheria Masaju.
Lissu aliongeza kuwa ameipata taarifa ya
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye alimwita mrithi wa Jaji Fredrick
Werema huku akimweleza kuwa ni mshauri wa serikali na si Bunge kuhusu
masuala ya kisheria ambapo Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Zungu alisimama
na kumtaka Lissu kutotumia lugha za vijembe badala yake ajenge hoja.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Masaju
alisimama kuomba mwongozo na kumtaka Lissu kuendelea kuheshimu mihimili
mingine kwa kutozungumzia mambo yaliyo mahakamani.
MTANZANIA
Bibi kizee anayekadiliwa kuwa na umri wa
miaka 70 asiyejulikana jina wala makazi yake ameanguka akiwa hajavaa
nguo yoyote nyumbani kwa mtu mkoa wa Shinyanga jambo ambalo limehusishwa
na Imani za kishirikina.
Suzana Mwandu ambaye ni mwenye nyumba
ambayo kikongwe huyo alianguka anasema alimkuta akiwa nje ya jiko llake
ambapo baada ya kumsemesha bibi huyo alizinduka na kuanza kuongea vitu
visivyoeleweka ambapo mashuhuda walihisi kwamba alikuwa akifanya
ushirikina.
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa Waziri Issa
amekiri kuwepo kwa tukio hilo ambalo lilikusanya umati wa watu ambapo
muda mfupi baadaye Polisi walifika na kumchukua ili kumnusuru bibi huyo
kupigwa na wananchi wenye hasira.
MTANZANIA
Mbunge Godbless Lema jana alimshambulia
kwa maneno makali Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi,
Paul Chagonja kuwa anaweza kuwa anashirikiana na majambazi wanaovamia
vituo vya polisi na kupora silaha.
Lema aliliambia Bunge kuwa Chagonja anaweza kuwa anahusika katika matukio ya ujambazi katika vituo vya polisi kwa sababu anataka kudhoofisha utendaji kazi wa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu huku akifananisha taifa na chumba kinachotumiwa na vijana wa kihuni kuishi ambacho hakina utaratibu.
Lema aliliambia Bunge kuwa Chagonja anaweza kuwa anahusika katika matukio ya ujambazi katika vituo vya polisi kwa sababu anataka kudhoofisha utendaji kazi wa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu huku akifananisha taifa na chumba kinachotumiwa na vijana wa kihuni kuishi ambacho hakina utaratibu.
“Mheshimiwa Mwenyekiti, geto ni mahali
ambapo watu wanaishi bila kufuata utaratibu, yaani katika geto, wakati
wa kulala anayewahi ndiye anayelala kitandani. Geto chakula kinapopikwa
kinaweza kuliwa hata kama hakijaiva, kwa hiyo nchi hii naifananisha na
geto kwa sababu watu wanaiba fedha za umma kama wanavyotaka…” Godbless
Lema.
“Katika ripoti za Bunge zilizosomwa hapa
jana (juzi) zimejaa wizi, kila ukurasa wa taarifa ya Zitto ni wizi tu,
wizi tu, hivi huu wizi utakwisha lini? Hata zile bunduki zinazoibwa
katika vituo vya polisi zinaweza kuwa ni ‘sabotage’ (hujuma),
zinazofanywa na Chagonja dhidi ya IGP,” alisema Lema.
Alisema amefanya uchunguzi wake binafsi
uliobaini kuwa Jeshi la Polisi limegawanyika na kwamba haamini kama Rais
Kikwete amekwishafanya mabadiliko ya uongozi ndani ya jeshi hilo.
Alisema ikitokea mawaziri wa Tanzania wakapelekwa nchini Tunisia wangeishachukuliwa hatua kali kwa sababu Serikali ya nchi hiyo haiwavumilii wabadhirifu wa fedha za umma.
Alisema ikitokea mawaziri wa Tanzania wakapelekwa nchini Tunisia wangeishachukuliwa hatua kali kwa sababu Serikali ya nchi hiyo haiwavumilii wabadhirifu wa fedha za umma.
MTANZANIA
Zitto Kabwe ni Mbunge wa Kigoma
Kaskazini na Mwigulu Nchemba, Mbunge wa Iramba Magharibi na pia Naibu
Waziri wa Fedha jana walialikwa kushiriki mahojiano katika kipindi cha
Jambo Tanzania kinachorushwa na Televisheni ya Taifa (TBC) ambapo
katika mjadala huo kila mmoja kumsifia mwenzake kwa utendaji kazi
uliotukuka.
Zitto alikwenda mbali zaidi kwa
kutangaza kumuunga mkono Mwigulu, ambaye amekuwa akitajwa kuwa mmoja wa
wanasiasa vijana wanaoendesha harakati za chini kwa chini za kuwania
urais baada ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza muhula wake wa pili wa urais
mwishoni mwa waka huu.
Katika mjadala huo, ni Mwigulu ambaye ni
mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyeanza kummwagia sifa Zitto
kwa jinsi ambavyo amekuwa akitekeleza majukumu yake ya kiuongozi katika
nafasi yake ya uenyekiti wa Kamati ya PAC.
Mwigulu alisema Zitto na kamati yake kwa
ujumla wamekuwa wakifanya kazi kubwa na nzuri ya kibunge na pia
kuishauri vizuri serikali na hasa Wizara ya Fedha.
Zitto alijibu pongezi hizo muda mfupi kabla ya kuhitimishwa kwa mjadala huo kwa kueleza kuwa iwapo Mwigulu ataonyesha nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa baadaye mwaka huu atamuunga mkono, kwa sababu ameonyesha kuwa ni kiongozi mzalendo na mwenye uwezo mkubwa wa kuelewa matatizo ya wananchi na kuyatafutia ufumbuzi.
Alisema ameamua kumuunga mkono kwa sababu yeye anabanwa na umri wake ambao unamwondolea sifa ya kikatiba ya kuwania wadhifa huo, tofauti na Mwigulu ambaye tayari amekwishatimiza miaka 40 inayotajwa kwenye Katiba kama moja ya sifa ya kumwezesha mtu mwenye nia ya kugombea urais kutekeleza matamanio yake hayo.
Alisisitiza kuwa uamuzi wake huo umetokana na tathmini aliyoifanya kuhusu mwenendo wa utendaji kazi wa Mwigulu ndani ya serikali ulioonyesha kuwa ana uwezo mkubwa wa kiuongozi.
Zitto alijibu pongezi hizo muda mfupi kabla ya kuhitimishwa kwa mjadala huo kwa kueleza kuwa iwapo Mwigulu ataonyesha nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa baadaye mwaka huu atamuunga mkono, kwa sababu ameonyesha kuwa ni kiongozi mzalendo na mwenye uwezo mkubwa wa kuelewa matatizo ya wananchi na kuyatafutia ufumbuzi.
Alisema ameamua kumuunga mkono kwa sababu yeye anabanwa na umri wake ambao unamwondolea sifa ya kikatiba ya kuwania wadhifa huo, tofauti na Mwigulu ambaye tayari amekwishatimiza miaka 40 inayotajwa kwenye Katiba kama moja ya sifa ya kumwezesha mtu mwenye nia ya kugombea urais kutekeleza matamanio yake hayo.
Alisisitiza kuwa uamuzi wake huo umetokana na tathmini aliyoifanya kuhusu mwenendo wa utendaji kazi wa Mwigulu ndani ya serikali ulioonyesha kuwa ana uwezo mkubwa wa kiuongozi.
Zitto na Mwigulu wameonyesha dhamira ya
kuunganisha nguvu zao ili kutekeleza malengo yao ya kisiasa, huku kukiwa
na mitazamo mbalimbali ndani na nje ya jamii kuhusu wanasiasa vijana
waliokwishaonyesha nia ya kuwania madaraka hayo ya juu ya Dola.
Kitengo cha jarida la The Economist cha
The Intelligence Unit ambacho hufanya ufuatiliaji wa siasa za kimataifa,
mwishoni mwa mwaka jana kilimtaja Zitto kuwa ni mmoja wa wanasiasa
vijana wa kambi ya upinzani ambaye nguvu za kisiasa.
The Intelligence Unit kilieleza kuwa
umaarufu wa kisiasa wa Zitto unatokana na nafasi yake ya kiongozi wa
kamati nyeti ya Bunge ambayo imekuwa ikiibua mambo mazito na yenye
athari katika taifa, hivyo licha ya kuwa na mgogoro na baadhi ya
viongozi wenzake ndani ya CHADEMA, bado anao ushawishi mkubwa wa kisiasa
kwa wadhifa alionao ndani ya Bunge.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment