Kumekuchablog
Tanga,ABIRIA wanaotumia uwanja wa ndege wa
Majanimapana Tanga, jana walilazimika kusubiria zaidi ya masaa matatu
baada ya kuzuka moto mkubwa katikati ya uwanja na kuchukua masaa 13 kuzimwa kwa
kusaidiana na wanafunzi wa Chuo cha Anga cha Kijeshi.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo ofisini kwake, Kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa
Tanga, Juma Ndaki, alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 8 mchana baada ya
wafanyakazi wa uwanja wa ndege kuona moto katika nyasi za uwanja sehemu ya
kurukia ndege.
Alisema moto
huo ulidumu kwa zaidi ya masaa matatu na
kulazimika kusitisha huduma za kutua na kuruka ndege jambo ambalo liliathiri
huduma za usafiri kwa wasafiri wa kisiwani Pemba na Unguja.
“Wafanyakazi
wa uwanja wa ndege waliona moshi mkubwa katika nyasi za katikati ya uwanja eneo
la kurukia ndege----moto ule ulikuwa ukisambaa kwa kasi na kuja eneo la jengo
ambako pia kuna ndege za mafunzo za kijeshi” alisema na kuongeza
“Baada ya
kuona moto ule ukizidi kushika kasi tulilazimika kuwaita wanafunzi wa Chua Cha
Anga cha Kijeshi na walisaidia kwa kiwango kikubwa lakini hivi ninavyozangumza
nanyi ndio tumeumaliza kuuzima wote” alisema Ndaki
Alisema
chanzo cha moto huo bado hakijajulikana na maofisa uwanja wa ndege na polisi
wanaendelea na uchunguzi na kusema kuwa hakuna mtu yoyote aliedhuriwa na moto
huo ambao ulikuwa unakimbilia maeneo ya makazi ya watu.
Alisema
kitisho kikubwa kilikuwa ni ndege za kijeshi ambazo zinakadiriwa kufikia 13
ambazo zimegesha uwanjani hapo ambazo ni za mazoezi ya kijeshi na kulazimika
kutumia nguvu za ziada ili moto huo kufika eneo zilipo.
Kaimu
kamanda huyo aliwashukuru wananchi wanaokaa kandokando ya uwanja huo kwa msaada
wao kwa kuweza kuudhibiti moto huo pamoja na kikosi cha zimamoto kuingia maeneo ya makazi yao.
Alisema kwa
sasa huduma zote zimerudi kama kawaida ikiwa na pamoja na safari za ndege
kuruka na kutua na kuviagiza vyombo vya usalama kuchunguza kwa makini tukio
hilo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment