Azuiwa kufanya mtihani kwa kufunga hijabu Canada
Mwanafunzi wa Kiislamu ameripotiwa kufukuzwa shuleni na kuzuiwa kufanya mtihani na mwalimu mmoja baada ya kukataa kuvua hijabu shuleni nchini Canada.
Tukio hilo lilizuwa utata baada ya kutokea kwenye shule ya upili ya College de Maisonneuve iliyoko mjini Montreal.
Msemaji wa shule hiyo Line Legare alitoa maelezo na kusema, ‘‘Mwalimu
wetu wa somo la biyolojia aliwahi kutangaza mwanzoni mwa mwaka kwamba
hatoruhusu wanafunzi wake kuingia kwenye mtihani wakiwa na kofia,
mtandio au hijabu vichwani. Mwalimu huyo alimfukuza mwanafunzi kutokana
na ukiukaji wa sheria iliyowekwa kwa hofu ya uwezekano wa kulaghai
kwenye mtihani.’’
Maelezo zaidi yamearifu kwamba mwanafunzi huyo alifukuzwa baada ya
kukataa kuvua hijabu kutokana na sheria za imani ya dini yake ya
Kiislamu.
Legare aliongezea kuwa tukio hilo limemkera mwalimu na hivyo basi,
wanaendelea kujadili ili mwanafunzi huyo aweze kufanya mtihani katika
tarehe nyingine.
Legare pia alisema kwamba mwanafunzi huyo bado hajawasilisha rasmi
mashtaka dhidi ya mwalimu na kwasasa utawala wa shule unafanya
mazungumzo ili kuhakikisha tukio kama hilo halirudiwi tena.
Kwa upande mwingine waziri mkuu wa mkoa wa Quebec Philippe Couillard
naye alitoa maelezo na kubainisha kuridhishwa kwa utatuzi wa mzozo huo
huku akiahidi kuwasilisha muswada bungeni kuhusu tukio hilo.
No comments:
Post a Comment